Basi yenye namba za usajili T 140 BGS Linalofanya safari yake kati ya Dar na Maundo Tandahimba likiwa limepinduka kufuatia kuchomoka kwa matairi ya mbele na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wengine zaidi ya 10 kujeruhiwa. Ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Sinza -Miteja wilayani Kilwa Mkoa wa Lindi barabara kuu ya Dar -Mtwara. Picha na na habari na Abdulaziz Video Lindi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 27, 2012

    Changamoto kwa waziri husika

    ReplyDelete
  2. Aina hii ajali inadhihirisha asilimia 100 kuwa tatizo ni ubovu wa basi lenyewe. Basi lililotengemaa haliwezi kuchomoka matairi kwa style hii!!!

    ReplyDelete
  3. Said Mwema aachie ngazi. Tezama basi hili tyres zilivyo vipara! Chini kumechakaa si kawaida. Police barabarani kazi kula mlungula tuuuuu! Hawajali usalama wa abiria wala wa raia kwa namna yeyote!! Tuko pabaya na Tunakwenda pabaya zaidi.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 27, 2012

    Hili basi au scraper?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 27, 2012

    Kama siyo mhandisi huwezi kukisia kwa karibu sababu ya hii ajali. Madereva acheni nyodo, jeuri na upuuzi. Jamii na matrafiq mnawaendekeza mno. Madereva wa Tanzania bara ni kaidi kuliko kokote nilikofika duniani, hata Reykjavik.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 27, 2012

    magari yanayoenda kusini hususan tandahimba,yamezidi kuwa mabovu,nnao mfano umenikuta mwenyewe,bus tumetoka nalo tadahimba mchuzi juu(.tanki la mafuta limetoboka,wameweka mafuta kwenye madumu )na tunapita kwenye vituo vya polisi,hawajali usalama wa raia,tunaiomba serikali ichunguze magari yanayoenda kusini,kwakweli ni mabovu tena sana,tusisubili kuona yaLIYIWAKUTA MV SKAGET ndo tuanze kutuma tume ya uchunguzi,magari yachunguzwe,ZUIA AJALI,EPUKA RUSHWA

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 27, 2012

    Mabasi siyo mabovu tu bali ni mikweche na kwa staili hii wengi wataumia na kufa.

    Askari wa Usalama barabarani wafanye uhakiki wa kila basi kama ni mkweche basi liyeyushwe na kuwa chuma chakavu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 27, 2012

    Wewe uliyepanda basi ambalo ni michuzi tupu na mkawapita polisi bila kusema na wewe hufai. Ulitaka nani akusemee. Ungewaeleza hao polisi mliowakuta njiani na kama wangepuuza ungekuwa umetimiza wajibu wa kuokoa maisha ya watu. Lakini ulikula jiwe kwa kuwa ulikuwa na shida. Usimlaumu mtu na wewe jilaumu kwani gari lingeanguka ukafa haya uliyoandika tusingeyajua wala kuyasikia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...