Mweyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje,Ulinzi na Usalama Mhe. Edward Lowass ( Mb) na Waziri Mkuu Mstaafu akisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Brigedia Generali, Dkt. Charles Muzanila kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) wakati wa kikao cha majadiliano na kubadilishana mawazo kilichofanyika siku ya pili ya ziara ya kikazi ya Ujumbe wa NUU. Mazungumzo hayo yalifanyika katika Makazi ya Balozi yaliyoko eneo la Dobbs Ferry.
Mkutano wa kubadilishana mawazo ukiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya NUU mara baada ya wajumbe wa Kamati hiyo kutembelea na kukagua majengo yanayomilikiwa na Serikali. Aliyesimama ni Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Esaka Mugasa, akijibu na kutoa maelezo kuhusu hoja zilizoulizwa na Mwenyekiti, Mhe. Edward Lowassa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 08, 2012

    Inakuwaje wabunge wafanye ziara wakati wa kikao cha bajeti? Hii si sawa iangaliwe upya.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 08, 2012

    Si tu wafanye ziara wakati wa bajeti bali pia wakati Taifa lipo kunako hatihati ya usalama wao Kiafya na hususan utabibu na matibabu!1 Hii hiingii akilini! Pls Mtua anisaide kujua hii imikaaje!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...