Kamanda Ras Makunja akiamrisha FFU wamwage m,abomu ya machozi |
Si wengine bali ni Kikosi kazi cha Ngoma Africa Band aka FFU,yenye maskani yake nchini Ujerumani bendi hiyo maarufu siku ya jumatano 12.9.2012 ilijikuta ikivaana jino kwa jino tena na washabiki sugu ndani ya juma la ajabu la "Klimahaus" Arena mjini Bremerhaven,Ujerumani.
Baada ya mdundo wa ngoma africa band kupenya katika nyoyo za washabiki wa mataifa mbali mbali walifurika katika onyesho hilo wengi wao wakiwa wenyeji wa ulaya.uwanja wa dansi ulionekana mdogo na kukawa na patashika la nguo kuchanika.
Washabiki waliodata akili walijikuta wakiperekana samba samba na muziki wa ngoma africa band, kiasi cha kuwafanya walinzi wa usalama kufanya kazi ya ziada kuhakikisha kila kitu kipo salama.
Ngoma Africa band aka ffu au maarufu kwa majina mengi ya utani kama vile "Watoto wa Mbwa" "wazee wa bongo tambarare" kutoka katika kabila la "Wagagagigikoko" waliogunduliwa katika MaaNdiko ya kitabu cha Buri Cheka watatumbuiza tena siku ya Jumamosi 15.09.2012 katika
Maonyesho ya AFRIKA_MESSE mjini Bremen,Ujerumani.
Usikose kuwasikiliza at www.ngoma-africa.com
si mchezo naona kamanda watasha wamekukaa kooni,hongereni sana ffu bin watoto wa wuh !wuh!
ReplyDeleteAnkal unikumbusha mbali kweli,hii kabila lao ffu? Wagagagigikoko unakikumbusha kitabu cha buricheka na adithi zake,ffu wanastaili kuwa na kabila hili na lugha yao ni virungu na vya machozi,Big Up FFU
ReplyDelete