Kamanda Ras Makunja akiamrisha FFU wamwage m,abomu ya machozi
 Si wengine bali ni Kikosi kazi cha Ngoma Africa Band aka FFU,yenye maskani yake nchini Ujerumani bendi hiyo maarufu siku ya jumatano 12.9.2012 ilijikuta ikivaana jino kwa jino tena na washabiki sugu ndani ya juma la ajabu la "Klimahaus" Arena mjini Bremerhaven,Ujerumani.

Baada ya mdundo wa ngoma africa band kupenya katika nyoyo za washabiki wa mataifa mbali mbali walifurika katika onyesho hilo wengi wao wakiwa wenyeji wa ulaya.uwanja wa dansi ulionekana mdogo na kukawa na patashika la nguo kuchanika.

Washabiki waliodata akili walijikuta wakiperekana samba samba na muziki wa ngoma africa band, kiasi cha kuwafanya walinzi wa usalama kufanya kazi ya ziada kuhakikisha kila kitu kipo salama.

Ngoma Africa band aka ffu au maarufu kwa majina mengi ya utani kama vile "Watoto wa Mbwa" "wazee wa bongo tambarare" kutoka katika kabila la "Wagagagigikoko" waliogunduliwa katika MaaNdiko ya kitabu cha Buri Cheka watatumbuiza tena siku ya Jumamosi 15.09.2012 katika
Maonyesho ya AFRIKA_MESSE mjini Bremen,Ujerumani.
Usikose kuwasikiliza at www.ngoma-africa.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. si mchezo naona kamanda watasha wamekukaa kooni,hongereni sana ffu bin watoto wa wuh !wuh!

    ReplyDelete
  2. Ankal unikumbusha mbali kweli,hii kabila lao ffu? Wagagagigikoko unakikumbusha kitabu cha buricheka na adithi zake,ffu wanastaili kuwa na kabila hili na lugha yao ni virungu na vya machozi,Big Up FFU

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...