Tulipokuwa tunaelekea mwishoni mwa wiki iliyopita,kuna jambo jipya lilikuwa linatokea. Jokate Mwegelo ambaye kwa wengi hahitaji utambulisho wa kina,alikuwa akizindua kampuni yake inayokwenda kwa jina la Kidoti Loving ambayo itajikita zaidi katika bidhaa mbalimbali zinazoendana na masuala ya urembo.Kwa kuanzia, Jokate alizitambulisha aina nane za nywele(weaving) ambazo Kidoti Loving tayari imeshaziingiza sokoni.
Baada ya pale nilimtafuta Jokate kuongelea zaidi Kidoti Loving na mengineyo. Fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo;

BC: Jokate,karibu tena ndani ya BC na naomba nianze kwa kukupa hongera nyingi sana kwa hatua uliyofikia ya kuzindua rasmi Kidoti Loving Brand.Hongera sana.

JM: Asante sana….. Nakumbuka mara ya mwisho kufanya interview na BC ni mwaka 2007….

BC: Kidoti bila shaka,na wewe mwenyewe umeelezea kwamba hilo jina linatokana na “birth-mark” uliyonayo hapo usoni kwako. Fine.Unakumbuka ni mtu gani wa kwanza kuanza kukuita kidoti? Na ilikuwaje ukafikia uamuzi wa kuiweka kidoti kuwa ndio brand name?

JM: Mtu ambaye naweza kusema ndio alichangia kwa mapana zaidi jina la “Kidoti” ni mdogo wake rafiki yangu wa karibu sana. Ilikuwa mwaka jana na nakumbuka nilikuwa kwenye pressure ya kutafuta jina la kuweka kwenye meza kwenye hafla ya Red Ribbon. Ilikuwa mara yangu ya kwanza kushiriki na mwandaaji mkuu wa Red Ribbon Gala,Khadijah Mwanamboka alikuwa akihitaji jina la designs zangu. Nikiwa kwenye pressure hiyo yule mdogo wake rafiki yangu ndio akaniambia kwanini usiziite Kidoti? Basi nikajikuta nasema tu zinaitwa Kidoti na kuanzia hapo ndio jina la Kidoti likawa rasmi na ndio mpaka sasa limeshazoeleka hivyo.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. OK Mungu akuzidishie
    Amekupa akili za kibiashara na pia sura na urembo
    Lakini kuna sababu ya kuvaa kivuli badala ya chupi? Vijana mnatuburuza katika mila za watu wengine na mnasahau sisi zetu mila na tabia.

    ReplyDelete
  2. hongera sana kidoti,nice shoes, ila vimembana hivyo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...