Tulipokuwa tunaelekea mwishoni mwa wiki iliyopita,kuna jambo jipya
lilikuwa linatokea. Jokate Mwegelo ambaye kwa wengi hahitaji utambulisho
wa kina,alikuwa akizindua kampuni yake inayokwenda kwa jina la Kidoti
Loving ambayo itajikita zaidi katika bidhaa mbalimbali zinazoendana na
masuala ya urembo.Kwa kuanzia, Jokate alizitambulisha aina nane za
nywele(weaving) ambazo Kidoti Loving tayari imeshaziingiza sokoni.
Baada ya pale nilimtafuta Jokate kuongelea zaidi Kidoti Loving na mengineyo. Fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo;
BC: Jokate,karibu tena ndani ya BC na naomba nianze kwa
kukupa hongera nyingi sana kwa hatua uliyofikia ya kuzindua rasmi Kidoti
Loving Brand.Hongera sana.
JM: Asante sana….. Nakumbuka mara ya mwisho kufanya interview na BC ni mwaka 2007….
BC: Kidoti bila shaka,na wewe mwenyewe umeelezea kwamba hilo jina
linatokana na “birth-mark” uliyonayo hapo usoni kwako. Fine.Unakumbuka
ni mtu gani wa kwanza kuanza kukuita kidoti? Na ilikuwaje ukafikia
uamuzi wa kuiweka kidoti kuwa ndio brand name?
JM: Mtu ambaye naweza kusema ndio alichangia kwa
mapana zaidi jina la “Kidoti” ni mdogo wake rafiki yangu wa karibu sana.
Ilikuwa mwaka jana na nakumbuka nilikuwa kwenye pressure ya kutafuta
jina la kuweka kwenye meza kwenye hafla ya Red Ribbon. Ilikuwa mara
yangu ya kwanza kushiriki na mwandaaji mkuu wa Red Ribbon Gala,Khadijah
Mwanamboka alikuwa akihitaji jina la designs zangu. Nikiwa kwenye
pressure hiyo yule mdogo wake rafiki yangu ndio akaniambia kwanini
usiziite Kidoti? Basi nikajikuta nasema tu zinaitwa Kidoti na kuanzia
hapo ndio jina la Kidoti likawa rasmi na ndio mpaka sasa limeshazoeleka
hivyo.


OK Mungu akuzidishie
ReplyDeleteAmekupa akili za kibiashara na pia sura na urembo
Lakini kuna sababu ya kuvaa kivuli badala ya chupi? Vijana mnatuburuza katika mila za watu wengine na mnasahau sisi zetu mila na tabia.
hongera sana kidoti,nice shoes, ila vimembana hivyo
ReplyDelete