MAHAKAMA ya Juu Kabisa nchini Kenya imeamua leo kuwa Uhuru Kenyatta alichaguliwa katika uchaguzi uliokuwa huru na wa haki,  na kutupilia mbali pingamizi lililowekwa na mgombea Raila Odinga aliyedai kwamba kura zilichakachuliwa na mashine za uchaguzi zilijaa kwikwi.
Uamuzi huo umesafisha njia kwa Uhuru Kenyatta kuingia Ikulu. Anatarajiwa kuapishwa wiki ijayo Aprili  9, 2013 uwanja wa michezo wa Moi.

Habari zimeingia sasa hivi zinasema aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Mhe Raila Odinga amekubali uamuzi wa mahakama kuu, na kukubali yaishe (shingo upande?) kuashiria kwamba sasa mambo ni tambarare, na sio kama ilivyohofiwa awali kuwa kutatokea vurugu kama za uchaguzi wa mwaka 2007.
“Ni uamuzi wa mahakama hii kwamba walalamikiwa wa tatu na wa nee walichaguliwa kwa haki”, alisema Jaji Mkuu wa Kenya Willy Mutunga, wakati wa kutoa uamuzi hu, akimaanisha Kenyatta na mgombea mwena na Naibu Rais William Ruto wameshinda kihalali.

Jaji Mkuu huyo alisema mahakama imetekeleza wajibu wake katika muda huo wa kihistoria. “Sasa ni juu ya Wakenya, viongozi wao, taasisi za kijamii, sekta binafsi na vyombo vya habari kutekeleza wajibu wao kuhakikisha umoja, amani, utaifa na maendeleo ya taifa vinahifadhiwa”, aliongezea.
Rais mteule wa Kenya huyo alimshinda mpinzani wake kwa asilimia 50.07 dhidi ya asilimia 43,28 za Odinga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. umepata taarifa vibaya - raila odinga hajakubali kwamba uchaguzi ulikuwa huru na wa haki sababu hakuridhika na uamuzi wa mahakama - amekubali yaishe tu

    ReplyDelete
  2. SASA RAIS UHURU AACHE POMBE!

    ReplyDelete
  3. "Doctored votes"

    David V

    ReplyDelete
  4. POLISI ANCHEKELEA WAKATI YUPO KAZINI. IS IT ETHICAL?

    ReplyDelete
  5. Kesi ya nyani kumpelekea tumbili unategemea nini?

    ReplyDelete
  6. Kweli kabisa hii ni kesi ya nyani kumpelekea ngedere, nchi za afrika hatutakaa tuendelee, sura yake inaonyesha tu kuwa ni mlevi bila hata kuuliza, kazi ipo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...