MAHAKAMA ya Juu Kabisa nchini
Kenya imeamua leo kuwa Uhuru Kenyatta alichaguliwa katika uchaguzi uliokuwa huru na wa haki, na kutupilia mbali pingamizi lililowekwa na mgombea Raila Odinga
aliyedai kwamba kura zilichakachuliwa na mashine za uchaguzi zilijaa kwikwi.
Uamuzi huo umesafisha njia kwa
Uhuru Kenyatta kuingia Ikulu. Anatarajiwa kuapishwa wiki ijayo Aprili 9, 2013 uwanja wa michezo wa Moi.
Habari zimeingia sasa hivi zinasema aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Mhe Raila Odinga amekubali uamuzi wa mahakama kuu, na kukubali yaishe (shingo upande?) kuashiria kwamba sasa mambo ni tambarare, na sio kama ilivyohofiwa awali kuwa kutatokea vurugu kama za uchaguzi wa mwaka 2007.
Habari zimeingia sasa hivi zinasema aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Mhe Raila Odinga amekubali uamuzi wa mahakama kuu, na kukubali yaishe (shingo upande?) kuashiria kwamba sasa mambo ni tambarare, na sio kama ilivyohofiwa awali kuwa kutatokea vurugu kama za uchaguzi wa mwaka 2007.
“Ni
uamuzi wa mahakama hii kwamba walalamikiwa wa tatu na wa nee walichaguliwa kwa
haki”, alisema Jaji Mkuu wa Kenya Willy Mutunga, wakati wa kutoa uamuzi hu, akimaanisha Kenyatta na
mgombea mwena na Naibu Rais William Ruto wameshinda kihalali.
Jaji
Mkuu huyo alisema mahakama imetekeleza wajibu wake katika muda huo wa
kihistoria. “Sasa ni juu ya Wakenya, viongozi wao, taasisi za kijamii, sekta
binafsi na vyombo vya habari kutekeleza wajibu wao kuhakikisha umoja, amani,
utaifa na maendeleo ya taifa vinahifadhiwa”, aliongezea.
Rais
mteule wa Kenya huyo alimshinda mpinzani wake kwa asilimia 50.07 dhidi ya
asilimia 43,28 za Odinga.
umepata taarifa vibaya - raila odinga hajakubali kwamba uchaguzi ulikuwa huru na wa haki sababu hakuridhika na uamuzi wa mahakama - amekubali yaishe tu
ReplyDeleteSASA RAIS UHURU AACHE POMBE!
ReplyDelete"Doctored votes"
ReplyDeleteDavid V
POLISI ANCHEKELEA WAKATI YUPO KAZINI. IS IT ETHICAL?
ReplyDeleteKesi ya nyani kumpelekea tumbili unategemea nini?
ReplyDeleteKweli kabisa hii ni kesi ya nyani kumpelekea ngedere, nchi za afrika hatutakaa tuendelee, sura yake inaonyesha tu kuwa ni mlevi bila hata kuuliza, kazi ipo
ReplyDelete