Waziri wa Ujenzi  Dr. John Pombe Magufuli (watatu kulia) na Balozi wa Denmark Tanzania  wakishuhudia utiaji saini mkataba wa ununuzi wa kivuko cha Dar Bagamoyo leo. Kivuko hicho kitajengwa na kampuni ya johs Gram-Hanssen A/S ya Denmark. Kivuko hicho kitakuwa na uwezo wa kubeba abiria 300 kwa pamoja na kinatarajiwa kukamilika miezi minane kutokea leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Kivuko cha Dar Bagamoyo? Au ni meli?

    ReplyDelete
  2. HONGERA MAGUFURI...WEWE NI JEMBE LA WATZ WANYONGE NA MASKINI! BIG UP!!!

    ReplyDelete
  3. meli ndio kivuko hau hujui nini mdau wa kwanza!

    ReplyDelete
  4. Hichi kivuko kitanunuliwa au kitajengwa? Ahaaa nimeelewa, hichi kivuko kitanunuliwa baada ya kujengwa! Ipo kazi, maana hata kikijengwa vibaya kitalalia kwako. Hivi Dar na Bagamoyo zimegawanywa na kitu kama mto hivi au bahari? eeh!

    ReplyDelete
  5. Wadau Kivuko ni umbali mfupi ambao hata kwa macho unaweza kuona upande wa pili ukikaa upande mmoja.

    Hapo wasiseme Kivuko ila waseme tu ''Mapango wa Usafiri wa Meli kati ya Dar na Bagamoyo''

    Sasa Dar hadi Bagamoyo panaonekana kwa macho?

    ReplyDelete
  6. Uneconomic viable:

    ''Mpango hauna tija Kiuchumi''

    -Pana uzalishaji gani utakuwa na tija kati ya Dar na Bagamoyo, au ni uzalishaji wa Machungwa wa Vijijini Kiwangwa na Gendagenda?

    -Bagamoyo pana viwanda vya uzalishaji mali hadi kupewa huduma za Vivuko na Meli?

    -Watalii kwa sasa Bagamoyo, idadi ni ndogo watalipa kama usafiri utatumika kuwasafirisha?

    -Kwa nini usiimarishwe usafiri wenye kipaumbele na tija Kiuchumi kwanza wa Meli kati ya Tanga na Dar?

    ReplyDelete
  7. Bora wangeweka Kivuko kati ya Dar kwenda Mafia!

    ReplyDelete
  8. hatua nzuri sana hongera pombe magufuri

    kivuko kitapunguza msongamano wa magari kati ya dar na bagamoyo wengi wetu tutasafiri kwa njia fupi ya baharini ili kupunguza msongamano huo

    jambo kubwa na lamuhimu ni kujitahidi usalama wa vyombo vya baharini ili tuweze kusafiri salama

    hatua nzuri sana maana wenzetu huku nchi zilizoendelea hutumia bahari kurahisisha mambo mengi sana mojawapo ni usafirishaji wa mizigo na watu kwa njia ya mkato

    naweza kutoa mfano kungelikuwepo na meli za kubeba vifusi n.k kwa wanaojenga kigamboni na mjini dasalame wangeweza kupata vifusi kutoka huko njia ya bagamoyo kwa urahisi zaidi.

    ReplyDelete
  9. Mbona kidogo sana? Hiki cha Magogoni kina uwezo wa kubeba watu 2000 na Magari kama 50. Hicho cha watu 300 hakilingani hata MV Kigamboni

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...