Waziri wa Ujenzi Dr. John Pombe Magufuli (watatu kulia) na
Balozi wa Denmark Tanzania wakishuhudia
utiaji saini mkataba wa ununuzi wa kivuko cha Dar Bagamoyo leo. Kivuko hicho
kitajengwa na kampuni ya johs Gram-Hanssen A/S ya Denmark. Kivuko hicho
kitakuwa na uwezo wa kubeba abiria 300 kwa pamoja na kinatarajiwa kukamilika
miezi minane kutokea leo.
Home
Unlabelled
mkataba wa ununuzi wa kivuko cha Dar-Bagamoyo watiwa saini leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



Kivuko cha Dar Bagamoyo? Au ni meli?
ReplyDeleteHONGERA MAGUFURI...WEWE NI JEMBE LA WATZ WANYONGE NA MASKINI! BIG UP!!!
ReplyDeletemeli ndio kivuko hau hujui nini mdau wa kwanza!
ReplyDeleteHichi kivuko kitanunuliwa au kitajengwa? Ahaaa nimeelewa, hichi kivuko kitanunuliwa baada ya kujengwa! Ipo kazi, maana hata kikijengwa vibaya kitalalia kwako. Hivi Dar na Bagamoyo zimegawanywa na kitu kama mto hivi au bahari? eeh!
ReplyDeleteWadau Kivuko ni umbali mfupi ambao hata kwa macho unaweza kuona upande wa pili ukikaa upande mmoja.
ReplyDeleteHapo wasiseme Kivuko ila waseme tu ''Mapango wa Usafiri wa Meli kati ya Dar na Bagamoyo''
Sasa Dar hadi Bagamoyo panaonekana kwa macho?
Uneconomic viable:
ReplyDelete''Mpango hauna tija Kiuchumi''
-Pana uzalishaji gani utakuwa na tija kati ya Dar na Bagamoyo, au ni uzalishaji wa Machungwa wa Vijijini Kiwangwa na Gendagenda?
-Bagamoyo pana viwanda vya uzalishaji mali hadi kupewa huduma za Vivuko na Meli?
-Watalii kwa sasa Bagamoyo, idadi ni ndogo watalipa kama usafiri utatumika kuwasafirisha?
-Kwa nini usiimarishwe usafiri wenye kipaumbele na tija Kiuchumi kwanza wa Meli kati ya Tanga na Dar?
Bora wangeweka Kivuko kati ya Dar kwenda Mafia!
ReplyDeletehatua nzuri sana hongera pombe magufuri
ReplyDeletekivuko kitapunguza msongamano wa magari kati ya dar na bagamoyo wengi wetu tutasafiri kwa njia fupi ya baharini ili kupunguza msongamano huo
jambo kubwa na lamuhimu ni kujitahidi usalama wa vyombo vya baharini ili tuweze kusafiri salama
hatua nzuri sana maana wenzetu huku nchi zilizoendelea hutumia bahari kurahisisha mambo mengi sana mojawapo ni usafirishaji wa mizigo na watu kwa njia ya mkato
naweza kutoa mfano kungelikuwepo na meli za kubeba vifusi n.k kwa wanaojenga kigamboni na mjini dasalame wangeweza kupata vifusi kutoka huko njia ya bagamoyo kwa urahisi zaidi.
Mbona kidogo sana? Hiki cha Magogoni kina uwezo wa kubeba watu 2000 na Magari kama 50. Hicho cha watu 300 hakilingani hata MV Kigamboni
ReplyDelete