Mbinu hii imefanikiwa kuthibiti wizi wa mfuniko wa barabarani kwa asilimia mia moja sasa kwani yapata mwezi sasa mfuniko huu uliopo mtaa wa Jamhuri jijini Dar es salaam una mwezi na ushee hivi haujachapwa.
Pongezi kwa waliobuni mbinu hii ambayo pia inatumika kama kip-lefti kwenye barabara hiyo nyembamba

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 16, 2013

    Hahahaaa hapo pana tundu kubwa ambalo ni hatari kwa watumiaji wa barabara. Lengo si kudhibiti wizi wa chuma chakavu. Anyways imesaidia kunusuru hicho kipande kilichobaki.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 16, 2013

    Hello ndugu zangu sio tuu NCHI yetu Tanzania hata huku niishio London mifuniko inaibiwa nakuuzwa kama chuma chakavu mbuni yanayo tumia ni kuweka mifuniko migumu ya plastic .. nchi yetu wamebuni mbuni hii ambayo nihatari zaidi ...

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 16, 2013

    kwa nini wasiweke mfuniko husikuwa wa chuma kuna mengine unaweza kutengeneza kwa zenge iliyochangwa na chuma..

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 16, 2013

    Ubunifu hapo ni SIFURI!

    Angalau wangechomea na WELDING kwa mbali kiasi kwamba ili kufanya wezi washindwe kuchukua.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 16, 2013

    Ni aibu kubwa saaana kwa sisi Wa-TZ kuwa wavivu wa kufikiri kufikia kiasi hiki.

    Hapo Ofisa amekaa Ofisini, ametafakari amevuta sigara labda akanywa na Pombe kidogo, ananyanyuka anapata jibu na akili hiyo, anawatuma Mgambo na matairi na matofali waende kuziba!

    Kama kutafuta mbinu za kufanya wizi wa Mifuniko ya vyuma barabarani usifanyike inatutoa kamasi, je tutaweza kutafuta mbinu za kukabiliana na changamoto mbalimbali NGUMU na TETE zaidi za Kimaisha?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...