Shirikisho  la Soka Tanzania (TFF) leo limejikuta likipata aibu ya mwaka baada ya Kampuni ya Flamingo Auction Mart, kuyapiga tanganyika jeki mabasi ya shirikisho hilo kutokana na deni la zaidi ya Sh.50 milioni wanalodaiwa na Kampuni ya Safina Holding ya jijini Dar es Saalam. 
Magari binafsi ya maofisa wa TFF wa TFF yakwia getini
Kampuni hiyo ya Flamingo  ilitia timu kwenye ofisi za shirikisho hilo kufuatia amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni ikitaka zoezi la ukamataji magari hayo hadi Juni 30 liwe limeshakamilika.
Fedha hizo za Safina Holding zimetokana na hifadhi ya baadhi ya timu zilizoshiriki michuano ya Kombe la Kagame mwaka jana na Yanga kuibuka kidedea. Magari ambayo yameamriwa na mahakama hiyo kukamatwa ni basi aina ya Yutong lenye namba za usajili T 581 CGR amoja na Toyota Mini Bus lenye namba za usajili T 528 ASJ. 
Lakini tofauti na amri hiyo ya Mahakama maofisa hao wa Flamingo walijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuingia kwenye mzozo na maofisa wa TFF na kuzuka zogo kubwa huku maofisa hao wa TFF kuzuia magari hayo yasichukuliwe.
Maofisa hao wa Flamingo wakiongozwa na Meneja Operation wao Noel Nyalila walitinga kwenye ofisi hizo na kulifunga gari lenye namba za usajili T 528 ASJ aina ya Coster na kulivuta kwenye gari lao lenye namba T 972 ABJ Jay Ambe, lakini walishindwa kuondoka nalo baada maofisa wa

Angetile Osiah akionesha barua yenye utata
TFF  kuzuia kwenye geti. 
 Wafanyakazi hao wa TFF waliamua kuzuia kwa kuegesha magari yao binafsi getini. Katibu Mkuu wa TFF Angetile Osia alisema waliamua kufanya hivyo baada ya barua ya  Mahakama alidai kuwa inaonyesha kwamba amri hiyo inapaswa kutekelezwa Juni 31 mwaka huu. 
 “ Tumelazimika kuzuia kwa sababu mwanasheria wetu amekwenda mahakamani ili kupata udhibitisho wa amri hii, kwa sababu tarehe ya kukamata magari haya ambayo ni Coster yenye namba T 528 ASJ na basi lenye namba T 581 CGR ni kweli tunadaiwa lakini tuna mpango wa kulipa,” alisema Osiah. 
Kwa upande wake Meneja Noel alisisitiza kwamba amri hiyo ni halali na wamefika hapo ili kuitekeleza kwa kuwa hukumu ilitolewa April 23 mwaka huu, amri ikaandikwa Juni 3 mwaka huu, ambapo June 31 wanapaswa kurejea mahakamani. Hata hivyo waliomba msaada wa Polisi ili waweze kusimamia kuyachukua magari hayo, na kufanikiwa
Basi la TFF likipigwa Tanganyika jeki

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2013

    Sio aibu kwa TFF tu, hata wenye "nembo" hiyo nyingine.

    Nani alaumiwe?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 06, 2013

    TFF. Walipe Deni. gari walipewa bure. Ni Lao

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 06, 2013

    Wote waliokaaa hapo ni wezi watupu we kila siku mnatangaza mamilioni ya viingilio hiyo milio 50 imekuwa kazi kulipa. Dawa ya deni ni kukulilipa hata kaaa kidogo kidogo. Ukiwafuatilia hao wana majumba ya kifahari kila kona ya mji. Shetwani tu hao.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 06, 2013

    Mbona Juni 31 hakuna kwenye kalenda, afisa ametoa toka kwenye kalenda ipi? Tuwe makini sana na utendaji wetu; najua umakini ni kasheshe sana nchi mwetu, ndiyo maana mikataba mingi na nchi za nje tunaburuzwa.

    ReplyDelete
  5. naaaam,hii inaonyesha jinsi gani TFF walivyo wababaishaji,mashindano alikuwa na wadhamini kwanini wajalipa mpaka leo,alafu tunasema TENGA na wenzake sio wababaishaji,wamezulumu mpaka leo pesa za kimbangulile,MUNGU amfichi MNAFIKI

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 06, 2013

    Hii ni aibu kwa wote TFF, NMB ambao walitoa magari hayo na nembo yao inaonekana na TBL wanaodhamini timu yetu ya taifa inayotumia magari hayo. Swali ni kwamba tangu 2011 TFF wanapata fedha toka ktk makato ya mechi mbali mbali na kwa Simba na Yanga pekee deni hilo lingemalizwa, fedha hizo zinakwenda wapi? je wanayo financial plan na wanao wataalamu wa fedha? Mambo yote haya yanatia mashaka makubwa. Ndio maana hawataki mtu asiyekuwa ktk kundi lao aingie ktk uongozi. wanafan.kata

    ReplyDelete
  7. Duh c mchezo. Bro Michu c aibu ya mwaka, ni ya Karne

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 07, 2013

    Mwanalibeneke liyepiga Picha za tukio hili Nampa Assalama Lekko zake!

    Hawa jamaa TFF na Uongozi mzima wanakuwa ni wajanja sana kukwepa na kutoa sababu na hija nyingi za kujitetea wanapobanwa.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 07, 2013

    Hapa ndio tunathibitisha ya kuwaUJANJA UJANJA NA WIZI UNAPOZIDI UTENDAJI mwisho wake ndio huu!!!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 07, 2013

    Hata kulipia madeni ya mabasi mmeshindwa?

    Nyomyi la Yanga na Simba mmeshindwa kulitumia mkalipa?

    Au mlitaka Raisi Kiwete awalipie hadi madeni ya mabasi?,,,hamwoni aibu ya kuwa Mhe. Raisi Alisha mlipa Maximo Mishahara hadi Mkataba wake unaisha akiondoka kwenda kwao Brazil!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...