Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo limejikuta likipata aibu ya mwaka baada ya Kampuni ya
Flamingo Auction Mart, kuyapiga tanganyika jeki mabasi ya shirikisho hilo kutokana na deni la zaidi ya
Sh.50 milioni wanalodaiwa na Kampuni ya Safina Holding ya jijini Dar es Saalam.
![]() |
Magari binafsi ya maofisa wa TFF wa TFF yakwia getini |
Kampuni hiyo ya Flamingo ilitia timu kwenye ofisi za shirikisho hilo kufuatia amri ya Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kinondoni ikitaka zoezi la ukamataji magari hayo hadi Juni 30 liwe limeshakamilika.
Fedha hizo za Safina Holding zimetokana na hifadhi ya baadhi ya timu zilizoshiriki michuano ya Kombe
la Kagame mwaka jana na Yanga kuibuka kidedea.
Magari ambayo yameamriwa na mahakama hiyo kukamatwa ni basi aina ya Yutong lenye namba za usajili
T 581 CGR amoja na Toyota Mini Bus lenye namba za usajili T 528 ASJ.
Lakini tofauti na amri hiyo ya Mahakama maofisa hao wa Flamingo walijikuta kwenye wakati mgumu
baada ya kuingia kwenye mzozo na maofisa wa TFF na kuzuka zogo kubwa huku maofisa hao wa TFF kuzuia magari hayo yasichukuliwe.
Maofisa hao wa Flamingo wakiongozwa na Meneja Operation wao Noel Nyalila walitinga kwenye ofisi
hizo na kulifunga gari lenye namba za usajili T 528 ASJ aina ya Coster na kulivuta kwenye gari lao lenye
namba T 972 ABJ Jay Ambe, lakini walishindwa kuondoka nalo baada maofisa wa
![]() |
Angetile Osiah akionesha barua yenye utata |
Wafanyakazi hao wa TFF waliamua kuzuia kwa kuegesha magari yao binafsi getini. Katibu Mkuu wa TFF Angetile Osia alisema waliamua kufanya hivyo baada ya barua ya Mahakama alidai kuwa inaonyesha kwamba amri hiyo inapaswa kutekelezwa Juni 31 mwaka huu.
“ Tumelazimika kuzuia kwa sababu mwanasheria wetu amekwenda mahakamani ili kupata udhibitisho
wa amri hii, kwa sababu tarehe ya kukamata magari haya ambayo ni Coster yenye namba T 528 ASJ na
basi lenye namba T 581 CGR ni kweli tunadaiwa lakini tuna mpango wa kulipa,” alisema Osiah.
Kwa upande wake Meneja Noel alisisitiza kwamba amri hiyo ni halali na wamefika hapo ili kuitekeleza
kwa kuwa hukumu ilitolewa April 23 mwaka huu, amri ikaandikwa Juni 3 mwaka huu, ambapo June 31
wanapaswa kurejea mahakamani. Hata hivyo waliomba msaada wa Polisi ili waweze kusimamia
kuyachukua magari hayo, na kufanikiwa
Basi la TFF likipigwa Tanganyika jeki
Sio aibu kwa TFF tu, hata wenye "nembo" hiyo nyingine.
ReplyDeleteNani alaumiwe?
TFF. Walipe Deni. gari walipewa bure. Ni Lao
ReplyDeleteWote waliokaaa hapo ni wezi watupu we kila siku mnatangaza mamilioni ya viingilio hiyo milio 50 imekuwa kazi kulipa. Dawa ya deni ni kukulilipa hata kaaa kidogo kidogo. Ukiwafuatilia hao wana majumba ya kifahari kila kona ya mji. Shetwani tu hao.
ReplyDeleteMbona Juni 31 hakuna kwenye kalenda, afisa ametoa toka kwenye kalenda ipi? Tuwe makini sana na utendaji wetu; najua umakini ni kasheshe sana nchi mwetu, ndiyo maana mikataba mingi na nchi za nje tunaburuzwa.
ReplyDeletenaaaam,hii inaonyesha jinsi gani TFF walivyo wababaishaji,mashindano alikuwa na wadhamini kwanini wajalipa mpaka leo,alafu tunasema TENGA na wenzake sio wababaishaji,wamezulumu mpaka leo pesa za kimbangulile,MUNGU amfichi MNAFIKI
ReplyDeleteHii ni aibu kwa wote TFF, NMB ambao walitoa magari hayo na nembo yao inaonekana na TBL wanaodhamini timu yetu ya taifa inayotumia magari hayo. Swali ni kwamba tangu 2011 TFF wanapata fedha toka ktk makato ya mechi mbali mbali na kwa Simba na Yanga pekee deni hilo lingemalizwa, fedha hizo zinakwenda wapi? je wanayo financial plan na wanao wataalamu wa fedha? Mambo yote haya yanatia mashaka makubwa. Ndio maana hawataki mtu asiyekuwa ktk kundi lao aingie ktk uongozi. wanafan.kata
ReplyDeleteDuh c mchezo. Bro Michu c aibu ya mwaka, ni ya Karne
ReplyDeleteMwanalibeneke liyepiga Picha za tukio hili Nampa Assalama Lekko zake!
ReplyDeleteHawa jamaa TFF na Uongozi mzima wanakuwa ni wajanja sana kukwepa na kutoa sababu na hija nyingi za kujitetea wanapobanwa.
Hapa ndio tunathibitisha ya kuwaUJANJA UJANJA NA WIZI UNAPOZIDI UTENDAJI mwisho wake ndio huu!!!
ReplyDeleteHata kulipia madeni ya mabasi mmeshindwa?
ReplyDeleteNyomyi la Yanga na Simba mmeshindwa kulitumia mkalipa?
Au mlitaka Raisi Kiwete awalipie hadi madeni ya mabasi?,,,hamwoni aibu ya kuwa Mhe. Raisi Alisha mlipa Maximo Mishahara hadi Mkataba wake unaisha akiondoka kwenda kwao Brazil!