Baadhi ya wakimbiza mwenge wa kitaifa na askari wa Mkoa wa Dodoma na viongozi wao wakipasha mwili kabla ya kuukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa viongozi wa mkoa wa Morogoro, Augosti 22, mwaka huu
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( kushoto) akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk Rehama Nchimbi ( kulia), baada ya kumaliza mbio zake katika Mkoa huo na kuanza rasmi Augosti 22, mwaka huu katika Mkoa wa Morogoro, makabidhiano  hayo yalifanyika kwenye mpaka kati ya Mikoa hiyo katika kijiji cha Ukwamani, kinachopatana  kati ya Wilaya ya Gairo , mkoani Morogoro na Kongwa , Dodoma, katika mkoa wa Morogoro unakimbizwa katika Halmashauri saba za Mkoa na kukabidhiwa Augosti 29, mwaka huu eneo la Bwawani, mpakani mwa wilaya ya Bagamoyo, mkoa wa pwani na Morogoro.

 Kikosi cha Sungusungu cha Tarafa ya Gairo kionesha umahili wake mapokezi ya Mwenge wa Uhuru.
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Kitaifa , Juma Ali Simai akinyosha mkono juu kuashiria kwa  wananchi na viongozi wa Mkoa wa Dodoma na Morogoro kuwa yenye yupi fiti kuendelea na jukumu la kuukimbiza mwenge wa uhuru hadi siku ya kilele , kabla ya mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk Rehama Nchimbi , kumkabidhi mwezake wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (  hayupo pichani ) jana ( Augosti 22) baada ya kumaliza mbio zake Mkoa humo ,makabidhiano  yaliyofanyika mpakani mwa  Mikoa hiyo eneo la  kijiji cha Ukwamani,katika  Wilaya ya Gairo , ya mkoa wa  Morogoro na Kongwa , Dodoma.
 Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa akimshikisha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Joel Bendera kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo kabla ya kuukabidhi kwa DC wa Gairo
 Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Mhe. Fatma Ally ( kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya mwenzake wa Bahi, mkoani Dodoma, Mhe. Betty Mkwassa 
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mhe. Anthony Mtaka ( kulia) akipokea mwenge wa Uhuru sambamba na Viongozi wengine wa Serikali wa Mkoa wa Morogoro. Picha na John Nditi wa Globu ya Jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Katika hii karne ya 21 nafikiri tunaweza kuja na a more sustainable development driven mwenge wa Uhuru. Tuupunguze wa kiserikali sana na kutoa fursa kwa watu binafsi na mashirika/ makampuni kuchangia kwa namna moja au nyingine. Inatakiwa Mwenge ukipita wakazi wote wawe wamehamasika. Shirikisheni makampuni ya events/ fundraising/ advertising wafanye bro bono.

    ReplyDelete
  2. akina Ras makunja nao wamo ! hawakosagi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...