Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akishiriki kuwasha mshumaa kama tendo la kuiangaza nchi ya Tanzania.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waumini wa kanisa la TGMIT lililopo Mwanza, Katibu wa NEC aliwaeleza waumini waliohudhuria ibada hiyo maalumu kuwa amani tuliyokuwa nayo imeletwa na Mwenyezi Mungu hivyo tusiruhusu ipotee.
Askofu Mkuu Msaidizi wa Kanisa la TGMIT Florence Ndaki akiongoza ibada maalumu ya kuiombea Tanzania amani, katika ibada hiyo viongozi mbali mbali walialikwa kutoka serikalini ,vyama vya siasa na asasi zisizo za kiserikali.
Waimbaji wa Kwaya maarufu nchini Martha Ramadhani na Mary Ruhasha wakiimba wimbo maalum wa kuitakia amani Tanzania kwenye ibada maalumu iliyofanyika leo tar.29 September 2013 kwenye knisa la TGMIT Mwanza.
Waumini wa Kanisa la TGMIT Mwanza wakiwa kwenye maombi maalum ya kuiombea Tanzania amani, ambapo Katibu wa NEC Itikadi na Unezi Nape Nnauye alikuwa mgeni mwalikwa na viongozi wengine kutoka serikalini,asasi zisizo za kiserikali na vyama vingine vya siasa.
mbona rushwa na kutokuwepo na haki ndo matatizo makubwa?
ReplyDeleteamani tulishapewa.
Haswaa, tena ni rahisi mno kutambua wapi tatizo lilipo.
ReplyDeleteTunapoomba amani maana yake hata hyo rushwa ni sehemu ya kuvunjika kwa amani. Kwa mantiki hyo tunaomba hata wala rushwa wajitambue .
ReplyDeletekwa sababu amani ipo tayari, hivi mtatathmini vipi kama sala yenu ni "effective"
ReplyDeleteMsitatue tatizo lisilopo wakati kuna matatizo mengi ya wazi.
Watu hawa wako sahihi kabisa maana wao wamesimama ktk msingi wa biblia maana neno halisi la amani katika biblia linaitwa "Shalom" ambapo linamaanisha:-
ReplyDeleteProsperity
Peace
Tranquility
welfare
Health
Safe
Rest
Friendly
hizi ndio maana za amani na amani inajumuisha kila kitu ndio maana MUNGU anaitwa MFALME wa AMANI
kwani tunaposema:-
Prosperity/mafanikio
(Je Kuna mafanikio kama kuna Rushwa?)
Friendly
(Je kuna urafiki mzuri na majirani zetu ikiwa hali ya mipakani si nzuri?)
Tranquility means "free from any kind of distabance" yani kuwa huru mbali na kuonewa pamoja na matatizo yote hata kuonewa kwa kukosa haki na pia majanga, njaa vita n.k
hivyo kuomba amani kwa anayeelewa maana halisi ya amani ni sawa na kuombea kila kitu hivyo mi naona watu hawa wapo sahihi kabisa na acha tuone nini kitatokea baada ya maombi yao ikiwa hali iliyopo itabadirika basi maombi yao ni "effective" na ndio chanzo cha mabadiriko.
Ahsante.
kilichofanywa na kanisa la tgmit was 100 percent correct, chochote kile kitafanyika kama amani ipo, even when we talk about politics hakuna politics kama hakuna aman, unajua hata watanzania wamepata uhuru wa kuhoji mambo kwa kuwa demokrasia yetu bado imejengeka katika aman na kuvumiliana, so guys we need to uphold peace.
ReplyDelete