Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akishiriki kuwasha mshumaa kama tendo la kuiangaza nchi ya Tanzania.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waumini wa kanisa la TGMIT lililopo Mwanza, Katibu wa NEC aliwaeleza waumini waliohudhuria ibada hiyo maalumu kuwa amani tuliyokuwa nayo imeletwa na Mwenyezi Mungu hivyo tusiruhusu ipotee.
 Askofu Mkuu Msaidizi wa Kanisa la TGMIT Florence Ndaki akiongoza ibada maalumu ya kuiombea Tanzania amani, katika ibada hiyo viongozi mbali mbali walialikwa kutoka serikalini ,vyama vya siasa na asasi zisizo za kiserikali.
Waimbaji wa Kwaya maarufu nchini Martha Ramadhani na Mary Ruhasha wakiimba wimbo maalum wa kuitakia amani Tanzania kwenye ibada maalumu iliyofanyika leo tar.29 September 2013 kwenye knisa la TGMIT Mwanza.
Waumini wa Kanisa la TGMIT  Mwanza wakiwa kwenye maombi maalum ya kuiombea Tanzania amani, ambapo Katibu wa NEC Itikadi na Unezi Nape Nnauye alikuwa mgeni mwalikwa na viongozi wengine kutoka serikalini,asasi zisizo za kiserikali na vyama vingine vya siasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. mbona rushwa na kutokuwepo na haki ndo matatizo makubwa?

    amani tulishapewa.

    ReplyDelete
  2. Haswaa, tena ni rahisi mno kutambua wapi tatizo lilipo.

    ReplyDelete
  3. Tunapoomba amani maana yake hata hyo rushwa ni sehemu ya kuvunjika kwa amani. Kwa mantiki hyo tunaomba hata wala rushwa wajitambue .

    ReplyDelete
  4. kwa sababu amani ipo tayari, hivi mtatathmini vipi kama sala yenu ni "effective"

    Msitatue tatizo lisilopo wakati kuna matatizo mengi ya wazi.

    ReplyDelete
  5. Watu hawa wako sahihi kabisa maana wao wamesimama ktk msingi wa biblia maana neno halisi la amani katika biblia linaitwa "Shalom" ambapo linamaanisha:-
    Prosperity
    Peace
    Tranquility
    welfare
    Health
    Safe
    Rest
    Friendly

    hizi ndio maana za amani na amani inajumuisha kila kitu ndio maana MUNGU anaitwa MFALME wa AMANI
    kwani tunaposema:-
    Prosperity/mafanikio
    (Je Kuna mafanikio kama kuna Rushwa?)

    Friendly
    (Je kuna urafiki mzuri na majirani zetu ikiwa hali ya mipakani si nzuri?)

    Tranquility means "free from any kind of distabance" yani kuwa huru mbali na kuonewa pamoja na matatizo yote hata kuonewa kwa kukosa haki na pia majanga, njaa vita n.k
    hivyo kuomba amani kwa anayeelewa maana halisi ya amani ni sawa na kuombea kila kitu hivyo mi naona watu hawa wapo sahihi kabisa na acha tuone nini kitatokea baada ya maombi yao ikiwa hali iliyopo itabadirika basi maombi yao ni "effective" na ndio chanzo cha mabadiriko.
    Ahsante.

    ReplyDelete
  6. kilichofanywa na kanisa la tgmit was 100 percent correct, chochote kile kitafanyika kama amani ipo, even when we talk about politics hakuna politics kama hakuna aman, unajua hata watanzania wamepata uhuru wa kuhoji mambo kwa kuwa demokrasia yetu bado imejengeka katika aman na kuvumiliana, so guys we need to uphold peace.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...