Kwa mara ya kwanza Siku ya ya Baba wa Taifa la Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere itaadhimishwa makao makuu ya Umoja wa Mataifa tarehe 14 mwezi huu. 
Shughuli hii imeandaliwa na ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa ambapo mwandishi wa idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa Joseph Msami (kulia), amefanya mahojiano na Mwakilishi wa Tanzania wake wa kudumu katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi na ameanza kwa kumuuliza ninini umuhimu wa siku hiyo? 

 (Mahojianao na Balozi Manongi) Shughuli hiyo itaenda sambamba na uzinduzi wa kitabu kiitwacho JULIUS NYERERE: Jabali wa Afrika katika medani za kimataifa kilichohaririwa kwa pamoja na Profesa Ali Mazrui na Dokta Linda Mhando. Hayati Mwalimu Nyerere alifariki dunia tarehe 14 Oktoba mwaka 1999 nchini Uingereza kutokana na ugonjwa wa saratani ya damu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. First at the UN kusherehekea Mwalimu! Bravo Tanzania. Keep it up!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...