Rais Jakaya Kikwete akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi Chuo cha VETA cha Wilaya ya Makete tarehe 19.10.2013 kilichojengwa katika Mji wa Iwawa, Makao Makuu ya wilaya hiyo. KatIka hafla hiyo uongozi wa Chuo hicho umeamua kukipa jina la Jakaya Kikwete kwa jitihada zake alizowezesha wilaya ya Makete kuwa ya kwanza nchini kuwa na chuo cha VETA cha wilaya. Kulia kwa Rais Kikwete ni Waziri wa Elimu NA Ufundi Dr. Shukuru Kawambwa na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Makete Ndugu Josephine Matiro.
Rais Jakaya Kikwete akifuatana na Mkewe Mama Salma wakitembelea Chuo cha VETA cha Makete na kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na wanachuo wa chuo hicho mara tu baada ya kukizindua rasmi tarehe 19.10.2013. 
Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma wakipata maelezo ya namna gani ya kupata udongo unaofaa kwa ajili ya kufyatua matofali kutoka kwa Geofrrey Sanga na Abel Mbilinyi, wanachuo wa mwaka wa kwanza wa chuo hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ankali huko wilaya za Wangingombe na Makete, mkoani Njombe hali ya hewa ipo nyuzi sentigradi nganimwezi huu wa Oktoba, maana ktk taswira naona mavazi ni ya hali ya baridi kama Uswisi.
    Mdau
    Geneva, Uswisi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mwasilah Ally KuppaOctober 20, 2013

      Utandandawazi,ukoloni mambo leo nikasumba kwa viongozi wetu na wananchi dhana imejengeka vazi la suti ndiyo rasmi kwenye shughuli kubwa kama hiyo ya kutaifa which is wrong kwan wangetupia mashat ya vitenge yenye rangi mbali mbali za wanyama waliopo ktk hifadh zetu wange babuka ngozi.

      Delete
  2. Yaani mdau ukielekea maeneo hayo kuanzia Mufindi na Njombe huko usisahau kuweka kakoti hata ikiwa ni kipindi cha summer kwa kwetu (December mpaka February).

    Ukisahau itabidi ukatafute mtumba sokoni

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...