Rais Jakaya Kikwete akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi Chuo cha VETA cha Wilaya ya Makete tarehe 19.10.2013 kilichojengwa katika Mji wa Iwawa, Makao Makuu ya wilaya hiyo. KatIka hafla hiyo uongozi wa Chuo hicho umeamua kukipa jina la Jakaya Kikwete kwa jitihada zake alizowezesha wilaya ya Makete kuwa ya kwanza nchini kuwa na chuo cha VETA cha wilaya. Kulia kwa Rais Kikwete ni Waziri wa Elimu NA Ufundi Dr. Shukuru Kawambwa na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Makete Ndugu Josephine Matiro.
Rais Jakaya Kikwete akifuatana na Mkewe Mama Salma wakitembelea Chuo cha VETA cha Makete na kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na wanachuo wa chuo hicho mara tu baada ya kukizindua rasmi tarehe 19.10.2013.
Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma wakipata maelezo ya namna gani ya kupata udongo unaofaa kwa ajili ya kufyatua matofali kutoka kwa Geofrrey Sanga na Abel Mbilinyi, wanachuo wa mwaka wa kwanza wa chuo hicho.
Ankali huko wilaya za Wangingombe na Makete, mkoani Njombe hali ya hewa ipo nyuzi sentigradi nganimwezi huu wa Oktoba, maana ktk taswira naona mavazi ni ya hali ya baridi kama Uswisi.
ReplyDeleteMdau
Geneva, Uswisi.
Utandandawazi,ukoloni mambo leo nikasumba kwa viongozi wetu na wananchi dhana imejengeka vazi la suti ndiyo rasmi kwenye shughuli kubwa kama hiyo ya kutaifa which is wrong kwan wangetupia mashat ya vitenge yenye rangi mbali mbali za wanyama waliopo ktk hifadh zetu wange babuka ngozi.
DeleteYaani mdau ukielekea maeneo hayo kuanzia Mufindi na Njombe huko usisahau kuweka kakoti hata ikiwa ni kipindi cha summer kwa kwetu (December mpaka February).
ReplyDeleteUkisahau itabidi ukatafute mtumba sokoni