Habari zimetufikia muda huu zinasema msafara wa Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe umepata ajali ambapo gari la DPP limepata ajali na kupinduka baada ya tairi la mbele kulia kupasuka. Eneo Ni Bwanga  na msafara unaelekea Chato kutokea Geita. 
Habari zainasema  gari hilo  limeishainuliwa  na safari inaendelea.Chanzo cha ajali hiyo kinaelezewa kuwa ilikuwa kuwakwepa  watoto wawili waliovuka barabara ghafla na bila tahadhari. 
Dereva na Abiria wote akiwemo Mkurugenzi wa makosa ya jinai Mhe. Biswalo Mganga na msaidizi wake inasemekana wametoka salama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 14, 2016

    Pole zao. Ila habari inajichanganya, tairi la mbele kulia kupasuka au kukwepa watoto? Nadhani si vizuri kuandika sababu za ajali kwa kuhisi ni vema kusubiri uchunguzi wa wataalamu.

    ReplyDelete
  2. Chanzo cha ajari sijaelewa, kupasuka kwa tairi au kukwepa waenda kwa miguu. Service za haya magari Ni muhimu sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...