SERIKALI inatekeleza Programu ya miaka mitano ya Maendeleo ya Sekta ya Maji nchini (2016/21) ambapo pamoja na mambo mengine imekusudia kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji katika Miji Mikoa ya Mikoa kutoka asilimia 86 hadi 95.
Taarifa ya Serikali kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji inaonesha kuwa Idadi ya wateja waliounganishiwa huduma hiyo imeongezeka kutoka 405,095 mwezi Machi 2016, hadi wateja 432,772 mwezi Machi, 2017 ambapo asilimia 97 ya wateja hao wamefungiwa dira za maji ili kulipia huduma ya maji kulingana na matumizi.
Pamoja na ongezeko hilo la uzalishaji wa maji bado mahitaji ya maji ni makubwa katika maeneo ya Miji Mikuu ya Mikoa ikiwemo Jiji la Dar es Salaam, hatua iliyoilazimu Serikali kuwekeza katika miundombinu ya maji na kuzijengea uwezo mamlaka za maji ili kuongeza upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama katika Jiji hilo.
idadi ya maunganisho kwenye mtandao wa majisafi ya Jiji la Dar es Salaam imeongezeka kutoka wateja 155,000 mwezi Machi, 2016 hadi kufikia wateja 182,721 mwezi Machi, 2017, kutokana na kuongezeka kwa makusanyo ya maduhuli ya mauzo ya maji kutoka Tsh. Bilioni 7.1 Machi, 2016 hadi Tsh. Bilioni 8.3 Machi, 2017.
Jiji la Dar lina wakazi takriban milioni tano lakini cha kushangaza ninyi mnawateja wasiozidi laki mbili. Hii inaonyesha kwamba maji yenu hayawafikii wananchi ipasavyo. Msipo sambaza haya maji kwa wananchi DAWASA itapata hasara na mwishoe kufa kabisa. Ikifika 2020 lazima muwe na wateja wasiopungua milioni kwa DSM only otherwise you r going to FAIL DSM.
ReplyDelete