RAIA 19 wa China na watanzania sita wamepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka ya uhujumu uchumi.
Washtakiwa hao wanashtakiwa chini ya vifungu vya sheria ya uhamiaji, chini ya sheria ya watu ambao siyo raia wa Tanzania na uhujumu uchumi.
Mbele ya Hakimu Mkazi Huruma Shaidi washtakiwa hao walitajwa kuwa ni, Bo Song, Liu Yunley, Chen Chao Hui, Fu Zeng, Wu Hai Quing, Ke Qiu Fang na Frederick Kumalija.
Wengine Jing Jing Lin, Ku Liao, Yan Yan Geng, Chen Ying Gong, Salim Mahsein Al-Amry, George Elikana, Fatuma Songoro, Bhoke Mwita, Kelvin Ponela, Chen Gwandi, Lin Ben, Rui Guo, Lin Xiangqui, Chen Fa, Wan Li, Robert Mkini na Revocatus Mugisha.
Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali Patrick Mwita akisaidiana na Shedrack Kimaro alidai, kati ya Juni 1 mwaka 2017 na Mei 18 mwaka 2018 walitenda kosa la kwanza, ambapo wanadaiwa siku hiyo, chini ya sheria ya watu ambao siyo raia wa Tanzania, walitoa taarifa za uongo kwa lengo la kupata kibali cha kufanya kazi nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...