Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
MWILI wa aliyekuwa kiongozi wa upinzani wa Jamuhuri ya watu wa Kongo Etienne Tshisekedi ambaye pia ni Rais wa sasa wa nchi hiyo Felix Tshisekedi umewasili nchini humo leo baada ya kuhifadhiwa nchini Ubelgiji baada ya kufikwa na umauti takribani miaka miwili iliyopita.

Wanafamilia wameeleza kuwa kuwa mwili utawasili kutoka Ubelgiji na kuzikwa kwa heshima nchini humo, Etienne alifariki mwaka 2017 Februari huko Brussels huko Ubelgiji akiwa na miaka 84 na mwili wake kuhifadhiwa huko kwa wasiwasi wa kiusalama.
Imeelezwa kuwa mwili wake utazikwa kwa heshima na maandalizi ya mazishi hayo yamekamilika.
Mazishi hayo yatahudhuriwa na marais mbalimbali huku ikielezwa kuwa atazikwa kama shujaa.

Mwanaye wa kiume Felix Tshisekedi aliapishwa kuwa Rais wa nchi hiyi Januari 24 mwaka huu akifuata nyayo za baba yake ambaye alikuwa mkosoaji mkubwa dhidi ya dikteta Mobutu Sese Seko.

Uyo felix ambaye pia ni rais wa sasa? na alisha kufa kabla ya kuwa rais����
ReplyDelete