Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

WAENDESHA bajaji na bodaboda katika Jiji la Dar es Salaam na hasa eneo la Mnazi Mmoja ya Posta Mpya wameanza kurejea kwa kasi kuendelea na shughuli zao kama kawaida yao.

Kurejea kwa huduma za usafiri huo ni siku moja tu baada ya kumalizika kwa kwa Mkutano Mkuu wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC) ambao ulifanyika Agosti 17 na Agosti 18 mwaka huu katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Kwa kukumbusha tu Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kupitia kwa Kamanda wake Lazaro Mambosasa walipiga marufu usafiri huo kuingia kati kati ya Jiji hilo ili kupisha mkutano wa SADC.

Ambao ulianza kwa kutanguliwa na shughuli mbalimbali zikiwemo za maonesho ya bidhaa ya viwanda kwa nchi za jumuiya hiyo.Hata hivyo baada ya Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es Salaam kupiga marufuku usafiri wale wote waliokaidi walikamatwa na bajaji na bodaboda zao kushikiliwa na jeshi hilo na kwa mujibu wa Mambosasa alisema waliokaidi katazo lao watapelekwa mahakamani.

Michuzi Blogu leo Agosti 19,2019 imeshuhudia usafiri huo wa bodaboda na bajaji ukiwa umeanza kurejea na hata kwenye maeneo ambayo bodaboda waliondolewa baadhi yao wamesharudi.

Hata hivyo baadhi yao wameonekana wakiwa na hofu na kuamua kuficha pikipiki zao na pale anapotokea mteja wanachukua walikoweka na kuendelea na safari.

Baadhi ya waendesha bodaboda wamesema pamoja na kuondolewa kwenye maeneo yao waliyokuwa wanafanya shughuli za utoaji huduma ya usafiri wanaipongeza Serikali kwa kufanikisha mkutano huo na kumalizika kwa uslama na amani.

Wengine wamesema kuondolewa kwao kwenye maeneo hayo ambayo wamekuwa wakiyatumia kusubiri wateja wao(wasafiri) imesababisha kuyumba kiuchumi lakini hiyo haiwapi shida kwani wamerudi na mambo yatakwenda sawa kwa madai nia ya Serikali ilikuwa njema.
"Kwangu kipindi chote cha SADC niliona kama vile nipo likizo ya muda mfupi maana nilikuwa naamini tutarejea na kweli leo tuko kwenye maeneo yetu.Bado tunahofu huenda tukafukuzwa lakini angalau baada ya siku kadhaa leo nimeingia mjini na bodaboda yangu,"amesema mwendesha bodaboda eneo la Posta Mpya Juma Kingimali.

Hata hivyo Jeshi la Polisi halijatoa taarifa ya kuruhusu bodaboda na bajaji kurejea kwenye maeneo waliyokuwa wameyazuia kwa muda kupisha mkutano wa SADC.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...