Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw Geofrey Tengeneza (wa pili kushoto) akionyesha fulana maalumu ya mbio za Rock City Marathon msimu mwa mwaka 2019 kwa wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa mbio hizo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio, Bw Clement Mshana (wa pili kulia) Mratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International (CPI), Bw Kasara Naftali (wa kwanza kulia) Pamoja na muwakilishi kutoka Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Bi Ombeni Zavara.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio, Bw Clement Mshana (Kulia) akizungumza kuhusiana na maandalizi ya mbio hizo. Wengine ni pamoja na Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw Geofrey Tengeneza (Kulia kwake), muwakilishi kutoka Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Bi Ombeni Zavara (wa pili kushoto) pamoja Mshauri wa masuala ya Ufundi wa mbio hizo Bw John Bayo (Kushoto)

Waratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International (CPI), Bw Kasara Naftali (kushoto) na Bi. Irine Lyimo wakionyesha muonekano wa T-shirts na medali maalumu kwa ajili ya msimu wa mwaka 2019 wa mbio za Rock City marathon.
Mshauri wa masuala ya Ufundi wa mbio hizo Bw John Bayo (kushoto) sambamba na mmoja wa raratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International (CPI), Bi Irine Lyimo wakionyesha muonekano wa T-shirts maalumu kwa ajili ya msimu wa mwaka 2019 wa mbio za Rock City marathon.
Mojawapo ya medali zitakazotelewa kwa washiriki wa mbio za Rock City Marathon msimu wa mwaka 2019
Baadhi ya wakiambiaji (joggers) kutoka klabu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam wakifurahia muonekano wa Tshirts pamoja na medali maalumu kwa ajili ya mbio za Rock City Marathon msimu wa mwaka 2019 wakati wa hafla ya uzinduzi wa mbio hizo.



Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imeahidi kushirikiana na waandaaji wa mbio za Rock City Marathon ili kuhakikisha kuwa mbio hizo zinatumika vema kuutangaza utalii wa ndani hapa nchini.

Akizungumza hii leo jijini Dar es Salaam wakati wa unzinduzi wa msimu wa kumi (10) wa mbio hizo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bi Devota Mdachi, Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa TTB,Bw Geofrey Tengeneza alisema adhma hiyo inasukumwa na malengo ya mbio hizo ambayo ni kutumia mchezo wa riadha katika kutangaza utalii hususani katika Ukanda wa Ziwa.

Hafla hiyo iliyofanyika kwenye viunga vya ofisi za TTB jijini Dar es Salaam ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa mchezo huo wakiwemo viongozi wa serikali pamoja na wadhamini mbalimbali wa mbio hizo.

"Kwa kuzingatia uzito wa malengo ya mbio hizi nitamke bayana kuwa TTB tupo tayari kushirikiana na waandaaji wa mbio hizi kuhakikisha kwamba mwaka huu mbio hizi zinafana na zinavutia washiriki wengi zaidi hususani wa kimataifa,'' alisema Bw Tengeneza.

Zaidi, Bw. Tengeneza pia alithibitisha ushiriki wake Pamoja na viongozi waandamizi wa bodi hiyo kwenye mbio hizo zinazoratarajiwa kufanyika Octoba 20, mwaka huu kwenye viunga vya jingo la kibishara la Rock City Mall, jijini Mwanza ambapo washiriki wa mbio hizo watapita katika barabara mbalimbali za jiji hilo kabla hazijamalizikia katika viunga hivyo.

Mbali na ushiriki huo, Bw Tengeneza pia alitoa pongezo kwa mashirika mbalimbali yenye dhamana ya utalii hapa nchini ikiwemo la Hifadhi za Taifa(TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)kwa kuwa sehemu ya wadau wakubwa wa mbio hizo hizo.

"Ukanda wa Ziwa una vivutio vingi ambavyo sisi kama kama chombo chenye dhamana ya utalii lazima tuendelee kuvitangaza kwa nguvu na kwa njia tofauti ikiwemo michezo,'' alisema Bw Tengeneza huku akivitaja baadhi ya vivutio hivyo kuwa ni pamoja na Kisiwa cha Saanane, Makumbusho ya kabila la Wasukuma pamoja na tamaduni za makabila ya wakazi wa Kanda ya Ziwa.

Mbio za Rock City Marathon zilizoanzishwa miaka kumi iliyopita zinazozidi kujiongezea umaarufu kila mwaka na tayari zimefanikiwa kuwavutia baadhi ya wadhamini ikiwa ni pamoja na kampuni za TIPER, Pepsi, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA).

Wadhamini wengine ni pamoja na kampuni ya uwakili ya Lis Law Chambers & Consultants, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), CF Hospital, Mwanza Water, Isamilo Lodge, Pigeon Hotel, Real PR Solutions Limited na Afrimax Strategic Partnerships Limited.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International waandaaji wa mbio hizo, Bw Clement Mshana alitoa wito kwa washiriki wa ndani hususani wa mikoa ya Kanda ya Ziwa pamoja na wadhamini kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mbio hizo ambazo kwa mwaka jana zilifanikiwa kuhusisha washiriki zaidi ya 3000.

Alisema mbio za mwaka huu zinatarajiwa kuhusisha washiriki wengi zaidi kutoka kila kona ya dunia ikiwemo Afrika, Ulaya, China, Mashariki ya Kati hususani Israel na Marekani huku akitoa wito kwa washiriki wa ndani kujisajili kwa wingi ili kuthibitisha ushiriki wao kwenye mbio hizo.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Mshauri wa masuala ya Ufundi wa mbio hizo Bw John Bayo alisema maandalizo ya mbio hizo kwasasa yamekamilika kwa asilimia 60 huku akitumia uzinduzi huo kuonyesha Tshirts na medali za zitakazotimika katika msimu wa mbio hizo kwa mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...