Na Karam Kenyunko, globu ya jamii.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeshindwa kuendelea na kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mmiliki wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power (IPTL), Herbinder Seth na Mfanyabiashara, James Rugemarila, kwa sababu mshtakiwa Rugemarila ni mgonjwa na hajaweza kufika mahakamani.

Hata hivyo, licha ya kwamba Rugemarila kuumwa bado kesi hiyo iko kwenye sintofahamu hususani juu ya Washtakiwa hao kuandika barua kwa  DPP wakitaka kufikia makubaliano jinsi ya kumaliza shauri lao.

Sintofahamu inakuja pale ambapo Sethi anadaiwa kuandika barua lakini hajawahi kuifahamisha mahakama kama ambavyo sheria inamtaka kufanya hivyo baada ya kuandika barua.

Mapema leo Oktoba 24,2019  Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi bado haujakamilika  na kwamba mshtakiwa Rugemarila anaumwa.

Hata hivyo baada ya maelezo hayo ya wakili Wankyo, ambayo hayakueleza   chochote kuhusiana na kinachoendelea kwa DPP,  mawakili wa utetezi nao hawakuzungumza chochote

 Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 7, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Seth na mwenzake Rugemarila wanakabiliwa na mashitaka  12 ya uhujumu uchumi  kwa kula njama, kujihusisha na mtandao wa uhalifu, kughushi nyaraka, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu,  kutakatisha fedha  na kuisababisha Serikali hasara ya USD  22, 198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...