Na Karama Kenyunko,Michuzi TV
MKURUGENZI Mkuu wa Bohari kuu ya Dawa (MSD) nchini, Laurean Bwanakunu na Mkuu wa Lojistiki wa bohari hiyo Byekwaso Tabura wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matano likiwemo la kuisababishia hasara ya zaidi ya Sh.Bilioni bilioni 3.8
Mashtaka mengine ni kuongoza genge la uhalifu, utakatishaji na matumizi mabaya ya madaraka. Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo leo Juni 5, 2020, na Wakili wa Serikali Faraja Nguka akisaidiana na mawakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Fatma Waziri na Sophia Nyanda mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Richard Kabati iimedaiwa kati ya Julai Mosi 2016 na Juni 30, 2019 katika maeneo maeneo tofauti jijini Dar es Salaam kwa washtakiwa hao wote waliongoza genge la uhalifu kwa lengo la kujipatia fedha.
Imeendelea kudaiwa kuwa, katika tarehe hizo hizo maeno ya Keko jijini Dar es Salaam kwa pamoja watuhumiwa hao waliisababishia MSD hasara ya Sh. Bilioni 3.8.
Katika shtaka la matumizi mabaya ya madaraka linalomkabili Bwanakunu, imedaiwa katika tarehe hizo hizo na eneo hilo hilo, kwa makusudi mshtakiwa alitumia vibaya madaraka yake kwa kuwalipa wafanyakazi wa MSD Sh. Bilioni 3.8 kama nyongeza ya mishara na posho bila kuidhinishwa na Katibu Mkuu wa Utumishi.
Aidha imedaiwa, siku hiyo, huko Keko jijini Dar es Salaam na maeneo mengine nchini Tanzania, washtakiwa kwa pamoja walihifadhi vibaya vifaa tiba na kusababishia vifaa hivyo vizisiweze kutumika kitendo ambacho kiliisababishia mamlaka hasara ya Sh. milioni 85.
Katika shtaka la mwisho imedaiwa, kati ya tarehe 1 Julai 2016 na tarehe 30 Juni 2019 huko Keko jijini Dar es Salaam washtakiwa kwa pamoja walijipatia Sh. Bilioni 1.6 huku wakijua kuwa fedha hizo ni zao la kosa tangulizi la kongoza genge la uhalifu.
Hata hivyo, washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 19, 2020 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa washtakiwa wamerudishwa rumande.
MKURUGENZI Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu mwenye shati jeupe n mwenzake Byekwaso Tabura, Mkuu wa Lojistiki wakiwa katika ukumbi wa wazi wa mahakama ua Hakimu Mkazi Kisutu wakisubiri kusomewa mashtaka yao katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili yenye mashtaka matano likiwemo la kuisababishia MSD hasara ya zaidi ya Sh. Bilioni 3.8
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...