ALIYEKUWA Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Bonde la Rufiji (Rubada), Aloyce Masanja, amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 14 jela baada ya kupatikana na hatia ya kosa la wizi wa Sh milioni 86.Pia, mahakama hiyo imemuamuru mshtakiwa Masanja kulipa fidia ya Sh. milioni 86 kwa kampuni mbili za kilimo zilizoingiza fedha kwa mshitakiwa huyo.
Hukumu hiyo imesomwa leo Septemba 16, 2020 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustina Mmbando wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mmbando amesema, mahakama umeridhika na ushahidi wa mashahidi watano wa upande wa mashtaka ambao wameweza kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa ni kweli mshtakiwa ametenda kosa.
Amesema, ushahidi uliotolewa mahakamani hapo, umebainisha kuwa kampuni mbili zilitakiwa kuingiza fedha katika akaunti ya Rubada lakini mshtakiwa alighushi na fedha hizo na kuziingiza kwenye akaunti yake ya kampuni ya Farm (T) Ltd.
Hakimu Mmbando ameongeza kuwa, mshtakiwa alikuwa mtumishi wa umma na ushahidi umebainisha kuwa alighushi nyaraka na kutaka fedha hizo ziingizwe kwenye akaunti yake binafsi badala ya kuingia kwenye akaunti ya Rubada.
"Mshitakiwa ndiye aliingia makubaliano na kampuni hizo na moja ya masharti ni fedha kuingizwa kwenye akaunti ya Rubada lakini Sh. Milioni 86 ziliingizwa kwenye akaunti ya Farm (T) Ltd licha ya kwamba Rubada ilitamka kwamba fedha hizo zimeingia kwenye akaunti zake jambo ambalo walikuwa wanajua sio kweli....., kama fedha hizo zingeingia kwenye akaunti ya Rubada kesi hiii isingekuwepo." Amesema Mmbando
Hata hivyo kabla ya kusomwa adhabu mshtakiwa alipewa nafasi ya kujitete ambapo aliiomba mahakama impunguzie adhabu, hilo ni kosa lake la kwanza, ana familia inayomtegemea na pia anasumbuliwa na ugonjwa wa kisukari.
"Baada ya kupitia ushahidi wote mahakama imebaini kuwa upande wa mashtaka umethibitisha mashitaka haya bila kuacha shaka kwamba mshitakiwa aliibia fedha za Rubadana hivyo umetiwa kwa mashtaka yote hivyo katola kila kosa utatumikia kifungo cha miaka 14 gerezani lakini adhabu itakwenda pamoja na utatakiwa kulipa fidia ya Sh milioni 86 na endapo wakishindwa, upande wa mashtaka utatakiwa kuuza mali za mshitakiwa ili walipwe.
Hata hivyo, upande wa utetezi umedai wanakusudia kukata rufaa.
Masanja anadaiwa kati ya Agosti mosi hadi 10, 2010 katika Jiji la Dar es Salaam, akiwa mtumishi wa umma na kwa wadhifa alionao aliiba Sh milioni 50 zilizofika kwake kulingana na nafasi yake ya ajira.
Pia alidaiwa kuiba sh. milioni 36 zilizofika kwake kulingana na nafasi yake ya ajira.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...