Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda (kushoto) akiwa na
Katibu Mkuu Kilimo Bw. Gerald Kusaya jana wakati wa kikao kazi na
Maafisa Kilimo toka mikoa na Halmashauri zote nchini kujadili
upatikanaji huduma za ugani jana ukumbi wa LAPF Dodoma.
Kaimu Mwenyekiti Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo
na Maji Mhe. Charles Mwijage (Mb) akizungumza kwenye kikao kazi cha
wizara ya kilimo na wataalam wa kilimo jana jijini Dodoma ambapo
amewapongeza wakulima na maafisa ugani nchini kwa kuhakikisha nchi
kwenye kipindi cha mwaka 2015 hadi 2020 kujitosheleza kwa chakula na
kutokuwa na njaa.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya akiwa
ameshika kijitabu kinachoonyesha Tozo, Ada na Kodi 105 zilizofutwa na
Serikali ya Awamu ya Tano katika Bodi na Taasisi zilizo chini ya
Wizara ya Kilimo mwaka 2015-2020 ili kuondoa kero kwa wakulima na
wawekezaji.Wizara imegawa nakala za vijitabu hivyo kwa Maafisa Kilimo
Mikoa 26 na Halmashauri zote 185 jana Dodoma ili wakaeleze mafanikio
hayo kwa wakulima.
Mwenyekiti wa Umoja wa Maafisa Ugani Kilimo (DAICOs) Bw.
Enock Ndunguru akizungumza kwenye kikao kazi na Waziri wa Kilimo jana
Dodoma ambapo ameomba wizara kutenga fdha za kutosha kuwezesha maafisa
ugani wa serikali kutekeleza majukumu yao hususan vijijini kama ilivyo
kwa sekta za elimu na afya.
Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda akitoa hotuba ya kufunga
kikao kazi cha siku mbili cha wataalam wa kilimo toka mikoa na
halmashauri zote 185 jana ukumbi wa LAPF Dodoma ambapo amesema wizara
yake katika bajeti ijayo itatenga fedha kwa ajili ya kuboresha huduma
za ugani ili kukuza tija ya uzalishaji.
Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda (aliyekaa katikati)
akiwa na watumishi wa Wizara ya Kilimo mara baada ya kufunga kikao
kazi cha wataalam wa kilimo wa mikoa na halmashauri jana ukumbi wa
LAPF Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...