Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeibuka kinara katika utoaji wa huduma bora za mawasiliano nchini, huku likieleza kuwa litaendelea kuwekeza katika miundombinu na mifumo ya huduma kwa wateja ili kuongeza ufanisi.

Taarifa hiyo imetolewa katika ripoti ya robo mwaka iliyosomwa na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angela Kairuki, ikieleza hatua mbalimbali zilizochukuliwa katika kuboresha huduma za mawasiliano nchini.

Akizungumza kuhusu maboresho hayo, Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Mbanguka, amesema uwekezaji katika miundombinu na mifumo umeiwezesha kampuni hiyo kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi, huku ikiimarisha mifumo inayorahisisha huduma kwa wateja kwa ufanisi na gharama nafuu.

“TTCL imekuwa kinara katika utoaji wa huduma bora za mawasiliano. Haya yote yanawezekana kutokana na miundombinu ambayo tumeiboresha zaidi, lakini pia uwekezaji katika mifumo ya ndani na mifumo ya nje ya namna ya kuwahudumia wateja wetu kwa urahisi na unafuu zaidi,” amesema.

Amesema TTCL itaendelea kuboresha miundombinu yake ili kuhakikisha huduma za mawasiliano zinawafikia wananchi katika maeneo mbalimbali nchini, sambamba na kuimarisha mifumo ya huduma kwa wateja.

Mbanguka amesema maboresho hayo yataendelea kutekelezwa kwa kuhakikisha mifumo inayosaidia utoaji wa huduma inawekwa na kukamilishwa kwa wakati, ili shirika hilo liendelee kutoa huduma bora, za haraka na zenye ufanisi.

Ameongeza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za TTCL katika kuimarisha huduma za mawasiliano nchini, huku ikilenga kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya wananchi na taasisi katika matumizi ya teknolojia na huduma za kidijitali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...