Na Said Mwishehe,Michuzi TV
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk Ashatu Kijaji, ameitaka TFS kukamilisha miradi ya Sh2.2 bilioni katika Hifadhi ya Msitu wa Pugu ifikapo Aprili 15, mwakani, kabla mashindano ya AFCON.
Dk Kijaji alitoa maelekezo hayo leo October 20, 2026 wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya miradi inayolenga kuboresha miundombinu na huduma za utalii katika hifadhi hiyo, ili iwe tayari kupokea wageni wakati wa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
Amesema fedha zote zilizoombwa na wizara kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya miradi hiyo zimetolewa na kusambazwa kwa taasisi husika, hivyo utekelezaji unapaswa kwenda sambamba na muda uliopangwa.
Waziri Kijaji amesisitiza umuhimu wa kukamilisha miradi hiyo kabla ya tarehe ya mwisho iliyowekwa, ili hifadhi iweze kutoa huduma zinazohitajika kwa wageni watakaotembelea Tanzania wakati wa mashindano hayo.
Uwekezaji huo unahusisha ujenzi wa nyumba za kulala wageni (cottages), ukarabati wa barabara na maandalizi ya maeneo ya mapumziko na burudani, yakiwemo sehemu ambazo wageni wataweza kukutana na kutazama mechi za AFCON katika mazingira ya asili ya msitu.
Akizungumzia maendeleo ya miradi hiyo, Naibu Kamishna Mhifadhi anayesimamia Kurugenzi Saidizi ya Huduma na Utawala kutoka Wakala wa Huduma za Misitu (TFS)Emmanuel Kibiko, amesema baadhi ya cottages zimekamilika kwa asilimia 100, huku nyingine zikiwa zimefikia wastani wa asilimia 70.
Amefafanua TFS imeanza pia maandalizi ya kujenga cottages nyingine saba, huku fedha za kutekeleza mradi huo zikiwa tayari zimetolewa.
“Tunatarajia kukamilisha ujenzi wa cottages hizo ifikapo Desemba mwaka huu ili kutoa nafasi kwa ukaguzi kufanyika Aprili 2027,” amesema Kibiko.
Kuhusu miundombinu ya barabara, amesema maboresho ya awali yamefanyika, huku fedha zilizotolewa zikitarajiwa kuwezesha ukarabati zaidi ili kurahisisha upatikanaji wa hifadhi hiyo, hususan wakati wa mvua.
Ameongeza kwa sasa Hifadhi ya Msitu wa Pugu Kazimzumbwi ina uwezo wa kuhudumia watalii wapatao 40, lakini uwekezaji unaoendelea unatarajiwa kuongeza uwezo huo na kupanua huduma za malazi, mapumziko na burudani.
Hifadhi hiyo yenye ukubwa wa takribani hekta 7,927 ni miongoni mwa maeneo yanayotumika kwa utalii wa mazingira. Uboreshaji wa miundombinu unalenga kuongeza mvuto wake na kuvutia wageni wengi zaidi kutoka ndani na nje ya nchi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti, ameipongeza TFS kwa kushirikiana na kamati za ulinzi na usalama katika kulinda misitu dhidi ya uvunaji na usafirishaji haramu wa mazao ya misitu.
Amesema ushirikiano huo ni muhimu katika kuzuia uharibifu wa mazingira na kuhakikisha rasilimali za misitu zinalindwa kwa manufaa ya wananchi na taifa.
Magoti ameahidi kuwa viongozi wa wilaya wataendelea kushirikiana na TFS na taasisi nyingine za Serikali kusimamia miradi ya maendeleo na kuhakikisha wanaokiuka sheria za uhifadhi wanachukuliwa hatua zinazostahili.
Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Wizara ya Maliasili na Utalii kuboresha miundombinu ya utalii nchini, sambamba na azma ya kufikia watalii milioni nane kwa mwaka ifikapo 2030.

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...