Na MWANDISHI WETU
HALMASHAURI ya Wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani, imeunda kamati maalumu itakayo saidia kukuza sekta ya uwekezaji ikiwa ni hatua ya kuongeza mapato kupitia sekta hiyo.
Kamati hiyo inayoundwa na watu sita imetangazwa leo katika Mkutano wa Robo ya Kwanza ya Mwaka wa Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Aidan Kitare, ameitaka kamati hiyo kufanya kazi kwa weredi, kuhakikisha Kisarawe inapaa katika sekta ya uwekezaji , kuinua mapato na kubuni vyanzo vipya vya ukusanyaji mapato hayo.
Kitare amesema, kutokana na usimamizi imara wa vyanzo vya mapato halmashauri hiyo inazidi kukua kwa kasi katika ukusanyaji ambapo ndani ya mwezi mmoja tu imekusanya zaidi ya sh. milioni 700 kutoka vyanzo vyake mbalimbali.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Nyahori Mahumbwe, amesema kamati hiyo itaongozwa na mwenyekiti wake Wakili Alkard Machumu, ambaye pia ni Ofisa Ardhi wa halmashauri hiyo na Katibu atakuwa Joakim Costa ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Uwekezaji Idara ya Maendeleo Biashara Viwanda wa halmashauri hiyo.
"Dar es Salaam sasa imejaa fursa za uwekezaji zipo mkoani Pwani. Hivyo tunalazimika sasa kupokea wawekezaji wengi wanaotaka kuwekeza hapa Kisarawe. Tunajiandaa kupokea wawekezaji hao kwa kuunda kamati hii ya uwekezaji,"amesema Mahumbwe.
Amesema kamati hiyo inawajibu wa kuandaa maeneo muhimu ya uwekezaji ambayo wawekezaji wanaweza kuwekeza bila kupata changamoto.
"Kwa mantiki hiyo kama kuna maeneo ya uwekezaji basi yanahusisha ardhi. Ardhi iwe imepimwa na kuthaminiwa. Tuhakikishe maeneo hayo hayana utata kwa wawekezaji. Ni aibu mwekezaji anawekeza kisha mwananchi anamshtaki mwekezaji,"amesema.
Amebainisha baada ya uundwaji wa kamati hiyo, kitaundwa kituo cha pamoja 'One Stop Centre' ya Kisarawe kurahisisha uwekezaji.
Amesema kituo hicho kitahusisha watalaamu wote kutoka taasisi zinazoguswa na masuala yanayo hususu uwekezaji.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati hiyo Wakili Machumu, amesema kamati yake itajikita kuangazia fursa za uwekezaji katika viwanda, utalii, hoteli, kilimo, ufugaji, michezo, burudani na elimu.
" Pia tutaanzisha Media kwa maana ya kituo cha radio na runinga. Wenzetu halmashauri nyingi wameanzisha na wamefika mbali,"amesema.
Amesma kamati imejiandaa kutembelea maeneo yote muhimu katika kata zote za wilaya ya Kisarawe kubaini fursa zilizopo.
"Uwekezaji mwingine ni katika maeneo kando ya misitu ambako tutajikita katika uwekezaji wa hoteli za kitalii, ujenzi wa ukumbi wa kisasa wa mikutano kituo cha mabasi .



.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)






.jpeg)

.jpeg)



.jpeg)
.jpeg)




.jpeg)




.jpeg)


.jpeg)












.jpeg)



.jpeg)
