November 2008
Kaka, Habari za safari?
Unapata internet wapi ukiwa vijijini? Au unatumia mitandao yetu ya simu? Natumia Zain nikiwa mikoani na inanisadia sana kitechnolojia. Niliahidi kutuma picha, nahisi hii ndio bora zaidi kutuma na sio zile nimepiga mbele ya Eiffel Tower. I feel this picture says something about France and Paris today.

Ukizoom, utaona kwamba ni picha hiyo hiyo moja, inayofanana na ya Obama wakati wa Uchaguzi US 08. Ila kila moja ina maandishi tofauti. Kauli mbiu ni YES WE CAN.

Maandishi yamenikumbusha matangazo ya shirika la HAKI ELIMU. Sijui kama ni chama chake kimeweka hizi poster mji mzima, lakini zinakumbushia ishu muhimu za kuzingatia kisiasa, kijamii, kiuchumi na fedha, kimazingira nk! Wanagusia AJIRA, RENEWABLE ENERGY, KODI KWA MAKAMPUNI YANAYOCHAFUA AU KULETA ATHARI YA MAZINGIRA nk.


Mwaka wa tatu ndani ya awamu ya 4, ni sahihi kiueledi kutathmini mwenendo wetu na sisi.

Katika vyombo vya habari, hapakosi kuwa na kipindi kuhusu nchi moja wapo za Afrika. Nchi hii bado ina ukaribu sana na yaliyokuwa makoloni yake. Hii ni kwasababu vijana wa sasa hawana uelewa mkubwa kuhusu watu weusi. Nao wamekua sehemu KAMILI ya jamii hii.

Watangazaji wa Kiafrika kwenye Tv ni wachache, au kwenye matangazo ya biashara, lakini timu yao ya mpira ni kielelezo kizuri cha DIVERSITE au mchanganyiko wa jamii ulaya leo!

Nilipostpone kutembelea Ubalozi hadi kesho asubuhi. Bado natafuta waungwana angalau niseme kiswahili kidogo kabla sijarudi Bongo wiki ijayo! Nawakilisha.
Safiri salama.
Taji Liundi
-------------------------
Taji!
Asante mdau kwa snepu na ujumbe mwanana. Naona Obama kakolea kila mahali. Ujumbe wake hata huku unatumika katika kuhamasisha mabadiliko katika jami. Kuhusu mtandao vijijini usikonde.
bongo siku hizi tambarare kwa jamu. Mtandao upo mradi tu kuwe na network ya nanihiii. Ah, si unajua tena. Mie bado nabangaiza vijijini. Raha kweli. Hakuna foleni ya magari wala nini.
Ukiazima injini kiuno kwa katibu kata wewe aaaaah unadunda tu. natamani kubaki huku wallahi. wenzetu hawana makuu, wanachapa sana kazi usiku na mchana. Halafu umoja ndio usiseme. Kila jambo linamhusu kila mtu.
Nakutakia ziara njema
-Michuzi

barbeque ya tembo
katika maandalizi
Kaka hiyo ni nyama ya tembo niliifumania kijiji kimoja ikikaushwa baada ya tembo huyo kuwindwa na watalii, hapo ni imebanikwa kwa ajili ya kuigawa kwa wakijiji woote wa eneo husika. Nilifanikiwa kuionja sijui wewe… Quality ya picha sio nzuri ni simu hiyo kaka.
Mdau John MnambaSalam Bro Issa Michuzi,
Ni Mpenzi na Mshabiki wa blog yetu ya jamii nikiwa naendeleza libeneke hapa Edinburgh Scotland Uk.
Kwa niaba ya Jamii ya watanzania waishio hapa tunaomba utupeperushie ujumbe wetu kwa jamii popote pale walipo ya ujio wa balozi wetu hapa edinburgh Napenda kuwakumbusha wanajamii wote kutembelea
na kujiunga na wanakijiji wa kibambaccm radio live Chini ni taarifa ya ujio wa balozi na nime attach card ya mualiko wa tamasha
Title: Launching of TzECA & Marking of 47th Anniversary of Tanzania Independence
Date: Friday December 5, 2008
Time: 7:00 pm - 12:00 am
Next reminder: The next reminder for this event will be sent in 3 days, 3 minutes.
Location: @ New Generation,
Newhaven Place,
Newhaven,
Edinburgh,
EH6 4LX
Phone: 07766176244
Notes: An opportunity to come together and celebrate launching of Tanzania Edinburgh Community Association and mingling with great supporters and friends of Tanzania
There will be African music, delicious African food will be on the menu, and all lots more. Come and start your weekend evening with us
Get your ticket quick to confirm your attending!!
To buy your ticket visit

Directions By Buses: Regular bus, Number 10 is the best one that takes you to the gate of Next Generation. Other buses are Number: 11 and 16 which are also both regular stopping at ASDA Newhaven, a walking distance to Next Generation.
NB:Please note that if you wish to attend this event (which should be great) and do not want to pay for a ticket online, you can send a cheque for £12 made out to 'Tanzania Edinburgh Community Association' and a stamped addressed envelope to:
c/o Dr Monica Mhoja
TzECA
10 Harvesters Square
Edinburgh
EH14 3JN.
Dr. Monica Mhoja will then send you your ticket.
Please do this as soon as possible!
Model RANGE ROVER
Year 2000
Type: Station Wagon 4 X 4
Mileage: 60,000 kms
Interior: Leather
Colour: Deep Dark Green
Petrol Engine
Extras : AC, CD Changer, Stereo, ABS, Sensors, Air Bags, Reclining Seats, Power Windows, Cruise Control, Automatic Elevation Control, Automatic Diagnosis System viewed on the dashboard panel.
CONTACT: (+255-754-411148)
mdau julius akiwa katulia rock city. chini na wadau wengine na ndani ya kirumba
Kaka michuzi,
hivi karibuni nilibahatika kusafiri nikafika rocky city leo umenitamanisha sana nilipoziona snap za jiji kwa kweli hata mimi nilivutiwa sana na mandhari ya jiji hilo.
kwa sasa tulibahatika kiungia kwenye wanja hilo maarufu la kandanda katika historia ya michezo East and Central Africapia nilichepuka nikaenda kandokando ya ziwa saa za jioni

Meneja wa Huduma za Jamii wa kampuni ya simu ya Zain Tanzania, Tunu Kavishe(kulia) akifafanua jambo kuhusu Zain inavyotoa huduma kwa jamii, kwa wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Denver kilichopo Colorado, Marekani wakati walipozuru ofisi za Zain ili kujua
shughuli mbalimbali za utendaji kazi zinavyoendeshwa katika kampuni hiyo, Dar
Meneja wa Huduma za Jamii wa kampuni ya simu ya Zain Tanzania, Tunu Kavishe(kushoto) akizungumza na wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Denver kilichopo Colorado, Marekani wakati walipozuru ofisi za Zain ili kujua shughuli mbalimbali za utendaji kazi zinavyoendeshwa katika kampuni hiyo, Dar
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya simu ya Zain Tanzania, Khaled Muhtadi (kushoto) akiwaeleza jambo wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Denver kilichopo Colorado, Marekani wakati alipotembelea ofisi za Zain ili kuona shughuli za utendaji kazi zinavyoendeshwa
katika kampuni hiyo, Dar

kijasti akiwajibika
Mambo vipi mdau wangu,

Mimi mzima kaka, kipindi hiki niko kwa watani wa jadi (Nairobi) nashiriki mradi wa animation. Mradi huu uko chini ya taasisi moja toka London inaitwa Tiger Aspect Production inashirikiana na kampuni moja ya kenya inaitwa Homeboyz.
Tunatumia michoro ya Tingatinga hivyo kuna wachoraji wa tingatinga 5, animator niko peke yangu!!!!!!!!!!!!!!!!!!. Wakenya zaidi ya 60 na wenyewe wadhungu kama 6 hivi.
Basically ulikuwa ufanyike Bongo ambapo wabongo kibao wangekula ajira kuanzia watu wa sound, wachoraji, magraphic artists, watu wa utawala, maakauntanti nk. Lakini wadhungu walipokuja kwenye survey miaka michache iliyopita wakakuta tuko kwenye mgao wa umeme wa kufa mtu.

unakumbuka ishu ya bwawa la Mtera?? machale yakawacheza, wakauhamishia Nairobari!!!! Ah Tanesko wamenyima wabongo ajira!!! Picha zaidi na maendeleo ya mradi huu wadau pia watembelee
Super model Sasha(Cutie Malisa) ni mrembo aliekuwa kileleni mwa mafanikio,nafasi ambayo kila mschana wa leo angependa kuwa nayo.

Pressure ya kazi pamoja na kutojiamini kunampelekea Sasha ajiingize katika utumiaji wa madawa ya kulevya hatimae mrembo Sasha anapoteza kila alicho kijali na kukipenda vikiwemo mumewe mpenzi Brian(Tito Zimbwe) ajira yake ya uanamitindo ambayo ndiyo iliyo muweka mjini Dar es salaam katika maisha ya kifahari na kumpatia umaarufu mkubwa.

Baada ya kukataa ukweli kwa muda mrefu Sasha anabaini kwa rafiki yake mpenzi Gabriella (Chuchu Hans) kama ameathirika na madawa ya kulevya na kukata tama ya maisha baada ya kukiri kuwa alijaribu kwa muda mrefu na kushindwa kuachana na tabia hiyo.

Jee Gabriella atachukua uamuzi gani kunusuru maisha ya Sasha? Ujio wa Mudrik(Khalfan Ahmed”Kelvin”) utabadilisha vipi muelekeo wa maisha ya Sasha?

Nini kitamfanya Sasha atambue kama umaarufu na urembo ni vitu vya kupita? Nini jamii itajifunza toka kwa mlimbwende Sasha?

KWA MAJIBU HAYO NA MENGINE MENGI JIPATIE NAKALA YAKO HALISI
FILAMU INA SUBTITTLES KATIKA LUGHA ZA
ENGLISH
FRENCH
ARABIC
PORTUGUESE
KWA WATEJA WA TANZANIA FILAM ZINAPATIKANA KATIKA MADUKA
YOTE YA FILAMU.
kwa wadau watakaopenda kununua wasiliana na
+447971224493

Mwasisi wa mziki wa reggae nchini Tanzania Jah Kimbute,atapanda jukwaani mjini Tempere,Finland,siku ya tarehe 7 February 2009 katika onyesho kubwa la aina yakeAfrica winter Jam festival.
Mwanamziki huyo nyota wa reggae Jah Kimbute pia atakuwa na ziara ya kikazi barani ulaya kuanzia February 2009.
Mwaandaaji wa onyesho hilo Bwana Mernard Mponda, amezitaja bendi zingine zitakazo shiriki onyesho hilo ni bendi maarufu barani ulaya The Ngoma Africa Band inayoongozwa na mwanamziki nyota Ebrahim Makunja aka ras Makunja yenye makao yake nchini ujerumani.
Pia Mwanamziki Lulu ya Tanzania Bi.Tabia Mwanjelwa ambaye kwa miaka mingi amekuwa kimya ataibuka katika katika onyesho hilo kwa kasi mpya!!!!!
Bendi ya Ngoma africa itawasili Tempere, Finland kwa kazi moja tu ya kuwatia kiwewe na kuwadatisha akili washabiki.
Jah Kimbute naye atatoa burudani ya aina yake kama walivyo mzoea washabiki wa scandinavia kwani sio mara ya kwanza kwa mwasisi huyo wa reggae kutumbuiza katika nchi hizo.
Tabia Mwanjelwa mwanadada wa Tanzania mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni na kuleta mafuriko ya washabiki amehaidi kutoa burudani ya aina yake
Wadau Finland kaeni mkao wa kula.
Habari ndiyo hiyo...
the debaters and moderator
prominent people from all over attended
CHADEMA chairman Hon. Freeman Mbowe prepares to leave after the session
Ayoub Mzee with Mzee Iddi Simba and CCM-London Chairman after the session

By Ayoub Mzee
www.ayoubmzee.blogspot.com
TWENTY years ago in the UK , when left-wingers were asked what kind of Scottish Parliament they wanted, they would reply: "A parliament with teeth."
It was a clumsy phrase, but they knew what they meant - a parliament with powers to intervene economically, particularly on jobs and industry.
The teeth were for taking bites out of the corporate fat cats.EPA,RICHMOND ? !
It looks like Tanzania Politicians have come up with their own version. This happened yesterday in London when Dr Harrisson Mwakayembe MP ,Vice chair ,Parliamentary Committee on Energy and Minerals, Idd Simba Chair Pride Tanzania , Hon. Freeman Mbowe ,Chair CHADEMA and Ludovich S.L Utouh the controller and Audit General were guests of the House of Lords in Britain to Launch their book-Bunge Lenye Meno.

The speeches revolved around Tanzania and its political stability, the relation ship between Development and Donor AID , the injustices at the global trading arena , the role of the opposition and issues about EPA and Richmond Scandals
Tanzania’s population possesses a high degree of political maturity and enjoys unfettered press freedom and a multi-party democracy.
Since gaining independence in 1961, the country has witnessed a peaceful democratic change in top leadership twice.

Once again this is evident when the speaker of Parliament Hon William Shija ,members from the opposition Like John Cheyo and CCM- the ruling party members have all contributed to a book ; which underpins political maturity and stability in the country .
Despite their political differences , their sense of political maturity is confirmed by their readiness to cooperate.

Speaker after speaker went on and on! Hard, were words spoken gently as a symbol of their FREEDOM.
SOFTLY like streams they broke forth , with no flags of retreat.
LOUD like a roll of thunder-STRIKE!.
The massage was got loud and clear in the corridors of power of England that the Tanzania of yesterday is not the Tanzania of todayJK akihutubi Mkutano wa awali kujadili zahama ya mfumo wa fedha duniani na jinsi ya kugharimia maendeleo duniani leo jijini Doha, Qatar
JK akihutubia mkutano wa awali kujadili zahama ya mfumo wa fedha duniani na jinsi ya kugharimia maendeleo duniani jijini Doha, Qatar, leo

JK akiteta na Mkurugenzi Mkuu wa World Trade Organisation WTO Director General Pascal Lamy jijini Doha, Qatar wakati wa mkutano wa awali kujadili zahama ya mfumo wa fedha duniani na jinsi ya kugharimia maendeleo duniani
JK akiongea na katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban-Ki moon wakiwa katika mkutano wa awali kujadili zahama ya mfumo wa fedha duniani na jinsi ya kugharimia maendeleo duniani huko Doha
JK wakibadilishana mawazo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban-Ki moon na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Balozi Augustine Mahiga huko jijini Doha leo
JK akisalimiana na Rais wa Sudan Omar al Bashir katika mkutano wa awali kujadili zahama ya mfumo wa fedha duniani na jinsi ya kugharimia maendeleo duniani

Na Mwandishi Maalum,

Doha, Qatar
Mkutano wa awali kujadili zahama ya mfumo wa fedha duniani na jinsi ya kugharimia maendeleo duniani, umekubaliana kuwa matatizo ya sasa ya mfumo wa fedha duniani ni dhahiri yataziathiri nchi zote duniani, tajiri na masikini na kuzidisha umasikini.

Mkutano huo pia umekubaliana kuwa ufumbuzi wa matatizo ya sasa katika mfumo wa fedha duniani ni lazima yatafutwe kwa pamoja na nchi zote kwa sababu hilo siyo jambo linaloweza kuachwa mikononi mwa nchi chache tu, hata kama zina uwezo kiasi gani.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambaye amehudhuria mkutano huo leo, Ijumaa, Novemba 28, 2008 mjini Doha, Qatar amesema kuwa mkutano huo umekubaliana kuwa katika hili nchi zote duniani lazima ziogelee kwa pamoja katika bahari ya matatizo hayo.

“Tumekubaliana kuwa lazima tuogelee pamoja kwa sababu kuzama kwa kila mmoja wetu siyo ni jambo lisilokubalika,” Rais Kikwete amesema baada ya kikao hicho kilichoitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki Moon.

Kikao hicho kimehudhuriwa na wakuu wa mataifa 20 yenye nguvu kubwa zaidi za kiuchumi duniani, taasisi za kimataifa za fedha pamoja na nchi chache zinazoendelea ikiwamo Tanzania.

Taasisi hizo ni Shirika la Fedha Duniani (IMF), Benki ya Dunia (WB) na nchi zinazoendelea ni Tanzania, Misri, Nigeria, Antigua, Norway, Kazakhistan, Philippines na Pakistan.

Rais Kikwete ambaye ameingia ukumbini kuhudhuria kikao hicho muda mfupi baada ya kuwa amewasili hapa jioni ya leo ameiwakilisha Tanzania na Afrika katika mkutano huo.

Mkutano wa leo ulikuwa wa utangulizi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Kimataifa Kujadili Jinsi ya Kugharimia Maendeleo Duniani na Jinsi ya Kukabiliana na Zahama za Sasa za Mfumo wa Fedha Duniani unaoanza kesho, Jumamosi, Novemba 29, 2008, kwenye ukumbi wa
Salwa.

Rais Kikwete amesema kuwa wakuu wa nchi katika mkutano huo pia wamekubaliana kuwa matatizo ya sasa ya mfumo wa fedha duniani yasitumike kupunguza utashi wa kisiasa duniani katika kupambana na athari za uchafuzi wa mazingira duniani na jitihada za kupambana na umasikini.

“Tumekubaliana vile vile kuwa pamoja na kwamba duniani inakabiliwa na zahama kubwa ya kiuchumi kutokana na kuvurugika kwa mfumo wa fedha duniani, bado hakuna taasisi ya kupambana na hali hiyo,” amesema Rais Kikwete.

Ameongeza kuwa utafiti unaonyesha pia kuwa matatizo ya sasa ya mfumo wa fedha duniani yataathiri na kurudisha nyuma jitihada za kufanikisha Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDG’s) kwa kiasi cha miaka saba. Malengo hayo yamepangwa kufikiwa mwaka 2015.

“Matatizo haya yatasababisha ukosefu mkubwa wa ajira. Yatawatumbukiza mamilioni ya watu, hasa katika nchi masikini zaidi duniani, katika umasikini mkubwa zaidi,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“Tusipokuwa waangalifu, matatizo haya yatasababisha zahama kubwa mno ya kibinadamu. Tunaweza kushuhudia watu wanarudi kwenye matatizo ya kichumi ya miaka ya 1930, wakati baadhi ya Wamarekani walipolazimika kuishi katika nyumba za maboksi.”

Ameongeza: “Ni dhahiri kuwa lengo la kupunguza umasikini duniani kwa nusu ifikapo mwaka 2015 kama MDG’s zinavyolenga litakuwa gumu mno kufikiwa kwa kutilia maanani matatizo ya bei za vyakula, bei za mafuta na matatizo ya mfumo wa fedha duniani. Yote haya, yanaongeza umasikini.”

Waziri Mkuu wa Msumbiji Mh. Luisa Diogo akisalimiana na Mama Maria Nyerere wakati alipomtembelea nyumbani kwake Msasani Jijini Dar kwa ajili ya kumjulia hali.
Waziri Mkuu wa Msumbiji Luisa Diogo akimvisha zawadi ya nguo aina ya kikoi Mama Maria Nyerere wakati alipomtembelea nyumbani kwake Msasani
Waziri Mkuu wa Msumbiji Luisa Diogo akibadilishana mawazo na Mama Maria Nyerere
Waziri Mkuu wa Msumbiji Luisa Diogo pamoja na wageni wengine wakitembelea bustani ya mboga ya Mama Maria Nyerere wakati walipomtembelea nyumbani kwake msasani Jijini Dar
Mama Maria Nyerere akimpa maelekezo Waziri Mkuu wa Msumbiji Luisa Diogo (aliyevaa nguo ya rangi ya udongo) kuhusiana na aina ya mboga iliyopo katika bustani yake. Picha na mdau Anna Nkinda wa Maelezo

Wadau wa Songea na vitongoji mnakaribishwa kwenye Tamasha la UKIMWI linalotarajiwa kufanyika katika Uwanja wa MajiMaji kesho Jumatatu Tarehe Desemba 1, 2008 kuanzia saa 3.00 asubuhi.

KARIBUNI WOOOOTE
Dk. Moses Ringo,
Mratibu wa Tamasha.

JK akiwa na Mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika Mh. Jean Ping
Heko JK, huu ndio utawala wa sheria
(Tahariri ya gazeti la Kulikoni la November 28, 2008)

MOJA ya sifa kubwa za Rais Jakaya Kikwete ni kutoonesha papara wala jazba katika maamuzi yake. Umakini na msimamo wake juu ya uongozi wenye kuzingatia utawala bora na sheria za nchi ulianza kuonekana wazi pale alipounda tume maalum ya Jaji Mussa Kipenka kuchunguza mauaji ya wafanyabiashara wanne wa madini.

Mauaji hayo yanadaiwa kufanywa na Polisi kwa amri ya aliyekuwa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam, Abdallah Zombe. Rais Kikwete hakuchelewa; baada ya kukabidhiwa ripoti ile na Jaji Kipenka, siku chache baadaye watuhumiwa wakatiwa mbaroni, akiwemo Zombe aliye rumande Gereza la Keko hadi leo akishtakiwa kwa mauaji.

Kama ofisa wa jeshi mstaafu, Rais Kikwete bado anakumbuka fika kwamba katika vita au mapambano yoyote kuna kushinda na kushindwa. Anafahamu fika kwamba kama ofisa wa jeshi wapiganaji anaowaongoza wanahitaji kuwa na ujuzi wa aina kuu mbili: Mikakati ya Mapambano (Military Strategies) na Mbinu za Medani au Stadi za Kivita (Military Manoeuvres).

Juu ya yote, anajua kwamba askari mzuri anatakiwa kuwa na afya njema, elimu na maarifa lakini katika mapambano kitu muhimu zaidi ni uvumilivu na subira. Katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake (2006-2008), Rais Kikwete ameonesha dhahiri tabia yake halisi ya uvumilivu na subira wakati akipanga mikakati ya kutekeleza mambo muhimu.

Mfano halisi ni jinsi alivyotoa matokeo ya ripoti ya ukaguzi wa hesabu za fedha za Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu Februari mwaka huu. Ukaguzi huo ulifanywa na kampuni ya Ernst & Young kwa niaba ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali na ripoti yake alikabidhiwa Rais.

Alikuwa na hiari ya kuitangaza au kuificha au kuibadili. Lakini aliamuru vyombo vya dola viwashughulikie wanasiasa, wafanyabiashara na maofisa waandamizi wa Benki Kuu waliohusika katika ufisadi ambao kampuni 22 zilichotewa bilioni 113/- za walipa kodi kwa wizi wa kughushi mwaka 2005 / 06.

Alisisimua umma wa Watanzania siku ya tangazo hilo lililoambatana na kufutwa kazi kwa Gavana wa Benki Kuu, Marehemu Daudi Ballali. Kwa niaba ya Rais JK, Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo alitangaza Februari 8, 2008 kwamba, Mwanasheria Mkuu Johnson Mwanyika, Inspekta Jenerali wa Polisi Saidi Mwema, na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Edward Hoseah wameagizwa kuchunguza na kuchukua hatua sahihi za kisheria, kinidhamu na kiutawala dhidi ya wahusika wote wa wizi huo.

Malalamiko, tuhuma za kulindana na mizengwe vilifuata na kupata upeo kila muda uliposogea huku umma ukiwa na shauku ya kuona mafisadi wanatiwa adabu kisheria. Wako waliobeza kwa kusema: “Ah, JK anatafuta umaarufu tu hakuna kigogo atakayeshtakiwa, mambo yataisha hivi hivi, tutasahau...”Lakini Rais wetu hakusahau mafunzo ya kijeshi sambamba na utawala bora. Alizingatia uvumilivu na subira.

Hata alipokwenda kuhutubia Bunge Agosti 21 mwaka huu alisema serikali imetoa hadi Oktoba 31 wezi wa EPA wawe wamerejesha fedha walizoiba. Alikuwa anavuta subira kuhakikisha kuwa wezi wanashtakiwa baada ya kurejesha mali walizoiba.Kiswahili kina methali zisemazo: “Mvumilivu hula mbivu” ; “Subira yavuta kheri”; “Kawia ufike” na “Heri kenda nenda, kuliko kumi nenda rudi”.

Hizo tatu za awali zinahimiza sana uvumilivu na subira ili kufanikiwa, lakini hiyo methali ya mwisho inahimiza zaidi uharaka katika maamuzi na utekelezaji, unapobaini uvumilivu na subira havina tija au vitaleta hasara.Rais JK alitumia busara hiyo.

Majalada ya watuhumiwa wa wizi wa EPA yalipelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka, na hatimaye Novemba 5 mwaka huu washtakiwa wa kwanza wa wizi huo wa kutisha wakafikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya jinai. Kila mwananchi makini sasa anajua faida ya uvumilivu na subira katika suala la EPA.

wamba asilimia 76.7 ya fedha zilizoibiwa zimerejeshwa na watuhumiwa wanapewa adabu inayostahili kisheria! Huo ndio utawala wa sheria unaozingatia umakini na busara.

Iwapo Rais Kikwete angekuwa na papara na kusikiliza shinikizo lenye jazba la kutaka wahusika wafikishwe mahakamani haraka, kiasi hicho kikubwa cha fedha zilizoibwa kamwe kisingepatikana.

Serikali nyingi duniani zimejikuta zikipoteza kiasi kikubwa cha fedha kutokana na hamaki ya kuwashtaki watuhumiwa na hatimaye kutiwa hatiani bila serikali kuambulia chochote. Wakati watuhumiwa wa wizi EPA wakiendelea kunaswa, Serikali ya Rais Kikwete haikubweteka kwa furaha na sifa kutoka kwa walipa-kodi na wapiga-kura wanaovuja jasho kila siku.

Jumanne ya Novemba 25 mawaziri wawili waandamizi katika Serikali ya Awamu ya Tatu, Basil Mramba na Daniel Yona, walipandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na mashtaka 13 ya jinai kwa matumizi mabaya ya madaraka na ofisi.Mramba alikuwa Waziri wa Fedha wakati Yona alikuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati wa muhula wa pili wa utawala wa Rais Benjamin Mkapa.

Wawili hao, kwa nyakati tofauti wakiwa madarakani, wanadaiwa kutumia vibaya madaraka yao kinyume na Ibara ya 96 (1) ya Sheria ya Makosa ya Jinai, Sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, hivyo kuikosesha serikali kiasi cha 11,752,350,148/- kutoka kwenye kodi.Kupelekwa kwa mawaziri hao mahakamani kulivuta hisia za Umma huku wengi wakisema msururu wa viongozi wote waliotumia vibaya madaraka yao ufikishwe mahakamani.

Lakini bado busara ya Serikali makini na Rais JK haziwezi kuruhusu papara katika maamuzi muhimu ya kisheria.Watuhumiwa wote wamepelekwa rumande baada ya kushindwa kulipa fedha taslimu bilioni 3.9/- taslimu kila mmoja. Kesi hiyo itatajwa tena Desemba 2, 2008, na upelelezi bado haujakamilika.

KULIKONI tunasema sasa umefika wakati umma wote umpongeze Rais Kikwete na serikali yake kwa hatua nzuri walizochukua na kumwombea kwa Mungu awaongezee busara wasisahau uvumilivu, subira, mkondo wa sheria, maadili ya uongozi, haki za binadamu na misingi ya utawala bora.
wadau Munir Shemweta Kulia) na Abdulwakil Saiboko wakiwa na mai dota wa Munir, Khairat, mara baada ya kula nondozzz zao za Shahada ya kwanza ya Mawasiliano ya Umma katika chuo kikuu cha waislamu Morogoro wikiendi hii.


tabia mwanjelwa akiendeleza libeneke huko ujerumani. chini ni tabia alivyo leo
Nani anayewezeza kubisha kuwa Mwanadada Tabia Mwanjelwa kuwa ni mwenye sauti hinayoweza kumtoa nyoka pangoni?

Tabia Mwanjelwa ni lulu ya watanzania iliyopotea kwa miaka mingi bila kusikika na kuwaacha washabiki wakiwa wanajiuliza yupo wapi?

Tabia mwanjelwa! wengine walifika hata kuvumisha na kuzua uzushi labda Tabia hatunayetena! Lakini majibu yanapatikana leo labda Tabia mwenyewe alishaimba kuwa: Maisha ni safari ndefu!!! Mwisho wa Maisha ni kifo!!!

Kwa bahati njema leo juhudi zimefanyika na bendi ya The Ngoma Africa inayoongozwa namwanamziki maarufu Ebrahim Makunja kuwa Lulu hiyo ya watanzania (Tabia Mwanjelwa)imeonekana !

kama kawaida ya watoto wetu wa uswahilini wanapookota kitu uimba Po! Changu! Po! Cha kuokota si cha kwiba!Cha Mchongoma Kina Mwiba!Lakini Lulu hiyo waliyoigundua Ngoma Africa wanairudisha mikononi mwa watanzania! wenyewe mpokeeni Tabia Mwanjelwa anarudi tena uwanjani kwa Kasi mpya! Nguvu Mpya!na miondoko mpya! kaeni mkao wa kula!

Tabia Mwanjelwa kwa sasa anaishi Ujerumani, mzima wa afya na sasa yupo studio kuwaletea nyimbo mpya ambazo kwa kiasi kikubwa zimesha kamilika.
The Ngoma Africa band wanampa shavu dada yao huyo kuhakikisha katika kila hali anarudi tena kwa kasi mpya.Tabia Mwanjelwa bado ana sauti yake utafikili kazaliwa leo! Mwanadada huyo LULU ya watanzania ni nguzo ya kuhaminika katika fani ya mziki.

no image
Familia ya Mheshimiwa Pius Msekwa inawaarifu ndugu, jamaa na marafiki kuwa kutakuwa na misa ya kumuombea mama yao mzazi aliyefariki 25.10.08 na kuzikwa 28.10.08 nyumbani kwake mlalakuwa Dar es salaam.
Misa hiyo itafanyika jumapili ya tarehe 7.12.08 katika kanisa la mtakatifu Anne
Gresham st
london EC2
kuanzia saa nane mchana.
wote mnakaribishwa na mungu amlaze mahali pema peponi.
asanteni
Watoto wa Marehemu Mama Erica Samwangwa Msekwa.
Bwana Michuzi,
Mimi Nimefurahi sana Kuiona hii blog yako, kwani kweli ni ya maendeleo.
Kuongelea maendele napenda niwataarifu Watanzania kuwa Wachina sasa wako tayari kununua mali kamili kutoka Africa.
Mali kamili namaanisha bidhaa ambazo zimetengenezwa na ziko tayari kutumika (Finished products). Miaka yote wamekuwa wakitaka tuwapatie bidhaa wazitengeneza (Yani RAW materials).

Nawasihi sana Watanzania wanotaka kujaribu biashara ya kuuza bidhaa zao China waangalie website hii
www.cantonfair.com
Hapa watapata maelezo yote ya jinsi ya kuingia na kuonesha bidhaa zao katika China Import Export Fair.

Hizo Picha ni mwaka huu mimi kwa niaba ya Multimodal nilishirika katika Maonesho hayo, kweli mafanikio ni makubwa.

Mwaka huu Kutoka East Africa Tulikuwa sisi wenyewe lakini kwa msaada wako bwana Michuzi nadhani watanzania wengi zaidi watanufaika mwaka kesho na miaka ijayo

Nakushukuru,

FREDDY MLAY
Branch Manager.
Multimodal Sourcing and Logistics Company LTD.
Guang yuan xi road,
Xiushan building 4th floor Room 4021.
TEL:+86 20 86508207
FAX:+86 20 86507207
CEL:+86 132 42807212 (8:00AM - 10:00PM CHINA TIME)
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kizuiani iliyoko Bagamoyo akipokea vitabu vya shule kutoka kwa afisa wa benki ya NBC Henry Nyondo vilivyotolewa na wafanyakazi wa benki hiyo mwishoni mwa wiki. Vitabu hivyo pia vitatumiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Nia Njema ya Bagamoyo pia. Katikati ni afisa elimu wa Bagamoyo Neema Robert na wa pili kulia ni Mshauri Masoko wa NBC Arden Kitomari.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Khanifa Karamagi (alievaa ushungi) akiwa na Mkuu wa Shughuli za Kibenki wa NBC Rajinder Singh na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Chanzige Victor Msoma katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa idara ya shughuli za kibenki ya NBC baada ya kukabidhi madawati 22 kwa shule hiyo iliyoko Kisarawe mwishoni mwa wiki.

Hizi taa za solar , zinatumia betri yenye kutumia mionzi ya jua , zinatengenzwa na WODSTA , (Women Development for Science and Technology Association ) huko Arusha. Hakuna haja ya giza kijijini jamani .

Hizo bulbu ndogo zinawekwa kwenye mfuniko wa chupa ya plastiki iliokuwa inahifadhi maji .( Recycled water bottles bulb covers ) System nzima ni betri ndogo inayodumu miaka mitatu na taa tatu .

Inagharimu kama $100 za kimarekani . Kwa kweli huwezi kulinganisha na gharama ya kuvuta umeme na bili za kila mwezi . Waliotaka kuwajengea mama zao au ndugu zao yale “majiko ya mama”

tuma email
kwa taarifa zaidi.

Muda umefika jamani wa kuunga mkono bidhaa zetu za kiTanzania zenye kustahili.
Mdau Msafiri SS
napiga mchi kijijini ng'wanswenhele katika kata ya iseni wilaya ya kwimba. hapo usipotwanga na na kupepeta unaweza kuula wa chuya.... mwanakijiji upo???
kliniki ya watoto kijijini hapo. hapo mtoto anadandia mzani na kubembea huku kazi ya kusoma vipimo ikiendelea. kwimba oye!


Mkuu wa wilaya na balozi nilikua safarini kidogo mitaa ya Peramiho nikaona nikupatie hii zawadi ya kikwangua anga cha peramiho kilichoanza kukwangua toka mwaka 1943. i think the Oldest kati ya vikwangua anga vya tanzania.Zawadi hii pia iwafikie wale wote wanaotokea maeneo hayo Mkoani Ruvuma.
Mdau na Mpenzi wa Masnep
Stewart