January 2006

huyu ndiye zakaria ndibameye, aliyekuwa mmiliki wa dar international orchestra ya marijani rajabu. kupata habari zake mpigie ismail wa mwenge jazz aliyekuwa katibu wa bendi ya dar international toka inaanza hadi inafifia. namba yake ni 0741 44 9852

jenerali banza stone mwana wa masanja akiingia ukumbini diamond jubilee na trupu lake la twanga pepeta kuzinduz albamu ya mtu pesa. hivi sasa twanga wako oman kwa ziara ya mwezi mmoja. wamembeba tena ali choki. banza na masfiri diouf wamebaki kwa sababu ambazo haziajaelezwa, ingawa watu wanasema banza na diouf wamesusa kwa kuwa choki karudishwa kwa dau kubwa kama mchezaji wa kulipwa!
no image
huyu ndiye zakaria ndabameye aliekuwa mmiliki wa bendi ya dar international orchestra chini ya jabali la muziki marijani rajabu. bw. zakaria hivi sasa anaishi kijijini kwake mjesani nnia ya kuelekea maramba huko tanga, akiwa hoi bin taabani, pamoja na kwamba bendi yake ilikuwa na nyimbo zipatazo 695 na albamu lukuki. ishukuriwe sheria butu ya hakimili ya tanzania ambapo mtu unaweza kuibiwa kweupeeee. enyi mlio ughaibuni, dili hili. ukiweza kuja na 'fomyula' ya kupambana na wizi wa hakimiliki umeula! muziki bongo sasa unashindana na unga! unaambiwa juma nature anaendesha benzi la dola 45,000, ana jumba la kifahari la milioni 150 na mapene kibao. na hapo anaibiwa!

kikosi kizima cha mabingwa wa soka tanzania bara dar young africans.
waliokaa toka shoto: ben mwalala, john baraza, nadir canavaro, dekilojo chambua (kocha msaidizi), jack chamangwana (kocha mkuu), abuu ramadhani, ahmed mkweche na edwin mukenya.

kati toka shoto: benjamin haule, mohamed banka, adbul mtiro, waziri mahadhi, maridadi bukenya, gaudence mwaikimba, yusuph khamis, amir kihemba, gulla joshua, andrew carlos, lulanga mapunda na mbarouk suleiman.

juu toka shoto: Deo lucas, shardack isajigwa, salum athumani, razak siwa (kipa wa makocha), suphian juma (daktari), herry morris, celdo mwaipopo, ramadhani wasso na said maulid.
no image
wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama ambao wamefanya kazi kubwa kuhakikisha bongo inakalika kwa amani na utulivu. kutoka shoto ni mkurugenzi wa usalama wa taifa cornel Apson, mkuu wa jeshi la polisi omar mahita na mkuu wa jeshi la wananchi generali george marwa waitara. hii ni kwa faida ya msiowafahamu watu hawa muhimu.

kushoto ni meya mpya wa jiji la dar alhaj adam kimbisa akikabidhiwa ofisi na meya aliyepita kleist sykes leo karimjee hall. kimbisa alipita bila kupingwa katika uchaguzi wa madiwani wa dar, ambapo sykes hakuwemo kwani alianguka kwenye kura za maoni mwaka jana, na nafasi yake ya udiwani kata ya kivukoni ikabebwa na huyu meya mpya, ambaye pia ni katibu mtendaji wa chama cha msalaba mwekundu tanzania.

mwalimu akicheza bao na mmoja wa wazee wa butiama huyu mzee ali hassan mwinyi, mama maria na kaka yake chifu burito wakishuhudia. napost picha hii nikiwa njiani kumtembelea mama maria, na kuona butiama ilivyo bila mwalimu. vile vile kesho jumamosi kanisa katoliki linamtukuza mwalimu (canonize) ikiwa moja ya hatua za awali za kumfanya mtakatifu. nimekosa usafiri hivyo siwezi kuwahi kwani shughuli hiyo yafanyika butiama saa nne jumamosi nami natua saa nane. hata hivyo kama kuna swali mtu angependa nimuulize mama maria aseme leo, ijumaa, nitamuulizia.

Huyu bibie ndiye kiongozi wa wa umoja wa kinamama wakimbizi katika kambi ya wakimbizi wa burundi ya mtabila, kigoma. hoteli hii marufu imeshahudumia hata marais na viongozi mbalimbali na wageni watembeleapo kambi hiyo. sina uhakika sheria ya hakimiliki ya majina inasemaje lakini usipokula sheraton mtabila uwapo huko una matatizo.

aidha hii ni mojawapo ya insha zangu nyingi zilizonipatia tuzo za uandishi uliotukuka. endapo kama mmependezwa nayo, ninazo nyingi kama hii, zenye 'human interest' na sio za kulenga viongozi kama ilivyo hulka yetu waandishi wa bongo.

siku moja moja huwa 'nawasha mwezi' kwa kutangaza ktk TV mbalimbali, hasa mambo ya michezo, hususan panapokuwa na michuano ya kombe la dunia ama la afrika. huwa nakuwa na mtaalamu dr. liki abdalla (kati) na mtangazaji wa kituo husika kama huyu wa TVT wakati wa kombe la ulaya mwaka juzi