Shkamoo kaka Michuzi na wanablogu wako kutoka pande zote za dunia.
Mi hua nimezoe kupita 2 kwa mbali ila leo nimeamua kugonga hodi na natumaini ntakaribishwa. Wabongo wana tabia yakuitana wakabila mtu anapojivunia anapotokea...mi sioni kama ni sawa that's why nikaamua kuandika kuhusu hiii mada!
Usiporinga utaishia KURINGIWA!
Siku zote mtu akisifia asili yake haswa kabila sometimes anaitwa MKABILA au MBINAFSI.Jiulize kama mtu hajaupathamani ukabila wake na kujivunia atafikia wapi kujivunia utaifa wake??Kama we huwezi kusema mimi ni MMASSAI,MJALUO au hata MMAKONDE kwa majivuno utafika sehemuuseme wewe ni MTANZANIA kwa majivuno???
Nikiwa bongomtu akiniuliza ''we mtu wa wapi?'' ntamjibu ''uchaggani'' bilakujali sifa mbaya tunazobambikiwa wachagga kwasababu napenda asili yangu.Nikiwa nje ya nchi ntajitambulisha kamaMtanzania even though tunaweza kujulikana kwa sifa ambazosio nzuri sana.Ukikaa na kufikiria sana tena kwa makini utagundua kwamba kila kitu kina faults,ziwe za kweli au la,watu wanazitilia maanani.
Utasikia....WAZUNGU ni wabaya(roho),wachoyo,wabinafsi...WAAFRIKA au watu weusi ni wezi,wakorofi,wajinga n.k.Sasa wewe utakataa sio mwafrikka kwasababu wanaitwa wezi???Labda unaweza ila hutakiwi kufanya hivyo,unatakiwa ujivune na una nafasi yakuonyesha kwamba wasemavyo SIVYO.
Mtanzania akiwa nje anajiskia raha sana kuongelea anapotokea(asili yake)...Tanzania this..Tanzania that!!Unaowaelezea wanakuita mtaifa au mbinafsi???I don't think so!Actually watakuona kama mzalendo anaependa, anaejali na kujivunia asili yake.Mtu wa maana ni yule anaeitambua thamani yake,anapotokea na kile alichonacho.
So the next time someone is proud of being from a certain tribe and ain't afraid of saying so,don't go around hating nakumwita mkabila.Kwanza kama hamjui,the fact kwamba Tanzania ina makabila mengi yenye mila na desturi ,lugha na sifa tofauti inafanya nchi yetu iwe na mvuto zaidi.Kama wote tungekua WAMASSAI nani angemu-admire mwenzake?.Nani angemtania mwenzake??Think about it.
Mimi ni MCHAGGA and I'm more than proud. Hata mkisema wachagga wezi na wanawake wanaua waume zao I don't care. I'm CHAGGA for life.
''YOU CAN ONLY ACHIEVE WHAT YOU GIVE YOURSELF CREDIT FOR''
Mwisho wa yote nakushukuru kaka Michuzi kwakupost mada yangu na wote walitumia muda wao wa thamani kusoma nilichokiandika.Kama kuna nilimuudha kwa namna yoyote ile, iwe kwakuchanganya lugha au kutetea ukabila naomba anisamehe sana.
By Lillian